Yaap, kama kawa mwanangu mwenyewe yaani kama nakuona vile
ilivyoitolea jicho safu hii kwa ijumaa hii tulivu, ila itakuwa mwake kiaina
kama baada ya kuusoma ukurasa huu ukalihifadhi gazeti lako ili siku ya siku
ujikumbushe kwa mara nyingine na kupitia mawili matatu, ila haiko poa kama
Dadangu pale uswazi mtoto haja kuu halafu wewe ukazolea ile kitu, sio swala la
kucheka sasa!
Oya, gwala kwa masela tulio kisongesha pamoko juzi ile
kwenye ka ukurasa haka na iko poa zaidi kwa wale mliotoa ushauri kupongeza na
mliouliza maswali na nikawajibu na kuwafafanulia kinaga ubaga kulingana na
maswali mliyo yauliza ila sina maana ya kwamba muendeleze maswali, mwisho wa
maswali ni ile juzi kati ok?
Tusonge sasa Mwana wane,
Katika meseji mbali mbali zinazosambazwa kupitia simu za
mkononi kuna moja kali sana, hii inawazungumzia wa Bongo na uvivu, tena hadi
kwenye mambo muhimu.
Kwa mujibu wa mtunzi wa meseji hiyo ni kwamba wabongo
kadhaa walivamia Benki kwa minajili ya kukomba mkwanja ambapo dhamira yao hiyo
ilifanikiwa kwa kiasi kinene na baada ya kukomba miburungutu wakafikanayo mafichoni wakiwa salama, lakini walipofika
mafichoni mmoja kati yao akawaambia wenzake.
“Oya, hela hizi nyingi mno ka’
vipi nyie endeleeni kuzihesabu mtaniambia kesho ziko shingapi.”
Umeicheki hii, kama hauja nisoma mwishoni utanisoma mwana,
iko hivi,
Mwishoni mwa miaka ya 90 bongo flavor ilikuwa juu sana kiasi
kwamba baadhi ya wasanii kama Profesa Jay,
Juma nature na wengineo wengi nyimbo zao zilikuwa ni mfano wa nyimbo za
taifa kwa jinsi zilivyokuwa zikipendwa mitaani na popote ambapo
zingesikika, ikiwa Profesa Jay alikuwa na wimbo mpya basi kila kona ya jiji
ungesikia watu wakisimuliana “Bwana umeisikia Ndiyo mzee, ni balaa.” Hata hivyo
hali hii ikaja kuzoeleka baada ya miaka kadhaa na baadaye ikaanza kuonekana ni
ya kawaida tu.
Lakini miaka ya 2000 akaibuka msanii Mjomba mpoto, huyu
mkali ingawa alikuwa na ngoma mbili tatu kabla lakini ngoma iliyomuweka pazuri
ilikuwa ni ngoma iliyosonga kwa jina la
‘MJOMBA’ kuanzia mistari ya ngoma
hii biti na hadi staili yenyewe ya uimbaji ikaitikisa nchi Serikali na raia
wake, huyu jamaa aliingia na staili kughani mashairi yake kwa kuongea ikapokelewa kwa mikono yote miwili.
Mchekeshaji maarufu hapa nchini wa kundi la Orijino Comedi
Mpoki alikuwa mfano wa wale wabongo niliowataja
pale juu ( wavivu ) hakutaka kuumiza kichwa badala ya kubuni staili na
mbinu za kuiteka jamii ya wapenda muziki yeye akaugeuza tu ule wimbo wa Mpoto, wake
akauita ‘SHANGAZI’ lakini kila kitu akafanya kama alivyofanya
Mpoto hata hivyo hili halikuwashangaza wengi kwani ni wengi tu wametoka kwa
staili za kukopi.
Mwaka uliofuata baada ya mpoki kukopi wimbo ule wa Mpoto
kulikuwa na tuzo za Kilimanjaro na katika wasanii waliokuwa wakigombea tuzo ya
muziki wa asili wawili hao ndiyo walikuwemo Mpoki kupitia wimbo wa Shangazi na
Mpoto kupitia Adela lakini hata hivyo Mpoki akaibuka kidedea na kunyakua tuzo
hiyo.
Baada ya kupokea tuzo hiyo akasema “HATA JOGOO ANAWAHI
KUAMKA LAKINI HAWEZI KUFUNGUA MLANGO.”
Kwa utashi wangu ni kwamba kijembe hicho alikuwa akipigwa Mpoto kwamba ni wa kwanza kubuni staili ya kuongea lakini ameshindwa kupewa
tuzo.
Kuna nilichobakiza?
Sasa, minasepa wanangu wenyewe hadi wiki nyingine, Adios!
No comments:
Post a Comment