POLENI WAPIGA KURA
Mpenzi msomaji samahani kwa kukucheleweshea hadithi hii kutokana na tatizo la umeme ofisini kwetu lakini naahidi kuwa juimatano ijayo itawahi. Mwandishi.
Imeandikwa na Shedrack Kilasi
Sithubutu na sito thubutu kufanya ujinga huo, sitaki nipige
halafu kesho na kesho kutwa nitamani mtu niliyempigia afe au aondolewe
madarakani kutokana na uzembe wake wa kuto waletea maendeleo watu na
kujinufaisha yeye mwenyewe kwa lasilimali za jamii husika kwani kumlaumu au
kutaka lolote baya limpate ili aachie ngazi itakuwa ni dhambi kwangu.
Nidhambi kuu pia kuwaacha wanangu wakikingojea kitumbua cha
kila siku halafu mimi nikaenda kupanga foleni kutwa nzima nikingojea kumpigia
kura mtu ambaye ataisaliti nchi yangu, atalisafisha jiji pindi tu atakapokuja
rais wa nchi kubwa ya Magharibi lakini baada ya siku kadhaa jiji litaendelea
kunuka na wananchi wake wa hali ya chini kufanya biashara hovyo kwenye vituo
vya mabasi na sehemu nyingine hatarishi.
Yap, dunia na taifa wanajua kwamba naichukia Siasa, hii
siasa ndiyo iliyomfanya Bibi na babu yangu wakafa bila kumsomesha mama yangu,
ni siasa hiyo hiyo iliyomfanya mama yangu akashindwa kuntusomesha na badala
yake akajiingiza kumshabikia mwanasiasa wa jimboni mwake na kumpigania mpaka
akapata Ubunge na kisha baadaye akawa Spika wa Bunge lakini siku ya kumsiba
wake hatukumuona na mbaya zaidi hakufanya lolote siku serikali ilipoamua
kuudhulumu ukoo wetu maeneo ya viwanja yaliyopo jimboni humo.
Lakini pia siipendi
Siasa kwakuwa inapingana na ukweli na nawachukia waumini wake kwakuwa
wameshawadanganya mno ndugu zangu wajinga, wakati mwingine na kaa na washkaji
maskani lakini wakianza kuongelea mambo
ya kuwasifia baadhi ya watu wa chama fulani naamua kuondoka zangu kwani naamini
hakuna cha afadhali, na ninasisitiza kwa chochote unachokifanya ukipata nafasi
ya kula kula tu ndugu yangu kwani kuna watu wanakula zaidi ya mnavyotegemea.
Huu ni ujumbe na ni maoni yangu tu sikulazimishi uamini vile
ninayoamini mimi ila mwisho wa siku nakushauri fanya mambo yako achana na mambo
ya siasa!
DIBAJI.
Ni miaka 20 tangu alipofariki mama yangu mzazi na tangu hapo
ndipo nilipoanza kuichukia siasa lakini kwakuwa nilikuwa mdogo nikataka
kupambana hadi mwisho ili kujua ni jinsi gani taifa langu linaangamia kwa uozo
huu wa viongozi wachache, haikuwa rahisi na kwa mawazo ya watoto wengi wa enzi
zangu naamini mimi nilikuwa ni gwiji kwakuwa juhudi zangu zilinifungua zaidi ya
msomi wa pale mlimani.
Kitu cha kwanza nilifikili kujiingiza kwenye vyombo vya
habari kwakuwa vyenyewe ndivyo vilivyokuwa vikiripoti matukio mengi ya siasa
ulaji rushwa na ufisadi, nikagundua pia kuwa wengi wa wanasiasa wenyewe hutokea
huku huku hili likaniaminisha kuwa ndani ya miaka 20 au zaidi nitakuwa na kitu
cha kuipa jamii…pakoje? Songa nayo
sasa!
Yap, kimya kimya mithili ya mtu akimbizaye mwizi baada ya
kufanya kazi kwenye vyombo vya habari kwa miaka 20 nikaachana nayo kwani ingawa ilikuwa hainilipi mimi nilikuwa
nikifanya uchunguzi wangu binafsi, ingawa kwenye ofisi niliyokuwa nikifanya
kazi watu walionizunguka walikuwa wamenizowea kupita kiasi lakini niliamua
kuipiga teke kazi hii ili kuelekea kulikomboa taifa langu masikini hivyo
kwakuwa nilikuwa na vyeti vinavyokubalika vya shule nikaamua kuingia jeshini
ambapo baada ya kukubaliwa nilijiunga na
jeshi na ndani ya miaka miwili nikaonekana ninakipaji cha kipekee na juhudio
kazini hivyo nikaulizwa kama nilihitaji kusomea ukomando kitu ambacho nilikuwa
nikikiwaza tangu siku naingia jeshini hivyo hata siku na kipingamizi ikawa
hivyo.
Miaka sita ilitosha mimi kukaa Urusi na baada ya kurudi
nchini Razam nilikuwa chimbo wakati huu wote mambo ya kishenzi yalikuwa
yakiendelea kutokea nchini mwangu ikiwa ni pamoja na ufisadi kuuawa kwa watu
wanaouliza ukweli au kuwa na uhakika wa kigogo aliyekula rushwa sanjali na
wakubwa kuruhusu meli za kuchimba mafuta kuingia nchini kinyemela huku wanachi
wakiamini ni mafuta ya Sample yaliyokuwa yakichukuliwa na meli hizo kubwa kila
leo.
No comments:
Post a Comment