Wednesday, October 22, 2014

MARI FC. YAPOKEA KICHAPO







Timu ya Mari Fc. Inayoundwa na kituo cha utafiti wa kilimo Mikocheni mwishoni mwa wiki ilikubali kipigo cha mabao mawili kwa nunge kutoka kwa timu ngumu ya Changanyikeni Veterani kwenye mtanange wa kirafiki uliopigwa kwenye nyasi za uwanja wa chuo cha Takwimu kilichopo maeneo ya Changanyikeni.
Iliwachukua dakika 30 pekee Changanyikeni kuandika bao la kwanza kupitia kwa Adam Mshamu ambaye alifunga bao hilo kwa njia ya penati baada ya beki wa timu ya Mari Fc Dk. Joseph Mdugara kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na mwamuzi Kasonta kuamuru lipigwe tuta.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikifanya mabadiliko ingawa mabadiliko hayo yaliinufaisha zaidi timu ya Changanyikeni Veterani ambapo kunako dakika ya 41 winga wa timu hiyo alipiga krosi safi iliyomkuta beki wa Mari Fc. Mwelam Mohamed na kuutumbukiza mpira kimiani wakati akijitahidi kuokoa.
Kocha wa Mari Fc.Zakaria Muyuyi Alisema vijana wake walijitahidi ingawa walizidiwa kidogo mbinu za kiuchezaji  na wachezaji wa timu pinzani lakini hata hivyo akasema kipigo hicho kimewapa changamoto kabla ya ziara yao ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Zanzibar.
Naye mzee wa timu hiyo Said Minazi Komba alisema timu hiyo ambayo inaongozwa na Dk.Joseph Mdugara licha ya ziara hiyo ya Zanzibar pia inajiandaa na mechi kadhaa za kimataifa ambazo zitapigwa nchini na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.