NIMESHIRIKI TENDO
LA NDOA NA MAMA YANGU MZAZI KISA UTAJIRI
Upepo
mwanana ukiwa ulivuma huku ukiambatana na milio ya Kunguru pamoja na Jogoo kuashilia kuwa kumekucha, ilikuwa yapata saa 12:30 asubuhi. kila
mtu akijiandaa kuelekea kwenye shughuli za ujenzi wa taifa. Ilikuwa ni
nyumbani kwa Mzee Lumbashi maeneo ya Mbezi Kimara mtaa wa Kinondo jijini Dar es salaam, Mzee Lumbashi alikuwa ni mjumbe wa serikali
za mtaa ambapo kulikuwa na umati mkubwa
wa watu uliotawaliwa na huzuni kubwa ya
msiba wa Mzee Lumbashi
aliyefariki dunia jana usiku katika hospitali ya taifa ya Muhimbili,
Mzee Lumbashi alikuwa akisumbuliwa na
tatizo la Kisukari kwa muda mrefu. Umati huu ulikuwa ukisubiri mwili wa
marehemu ambao ulikuwa bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika
Hospitali ya Muhimbili. Mnamo Saa 7:00
mchana mwili wa Mzee Lumbasi
uliwasili na baadaye ulipumzishwa
katika makaburi ya Kinondoni. Marehemu Mzee Lumbashi aliacha mke na mtoto mmoja
ambaye aliitwa Hamady. Hamady na mama
yake walihuzunika sana kwa kumpoteza mtu muhimu katika familia yao aliyekuwa
akitegemewa sana kwani alikuwa ni msaada mkubwa kwao, baada ya mazishi kila mhusika aliaga kwa
wafiwa na kurudi majumbani mwao
kuendelea na shughuli nyingine. Hivyo pale nyumbani walibakia Hamady na mama yake. Haikuwa rahisi kwa usiku ule
kwa hamady kupata usinginzi.
Hamady
alionekana mwenye mawazo sana akifikiria majukumu atakayokuwa nayo maana
alikuwa ni mtoto wa pekee kwa marehemu
Mzee Lumbashi, hivyo hakukuwa na mtu mwingine katika familia wa kuweza kusaidia
familia yao. Aliendelea kuwaza kwa muda
mpaka hapo usingizi ulipompitia na
kuweza kulala.
Ilikuwa yapata wiki moja sasa toka kuondokewa na baba yake, haikuwa rahisi kwa Hamady kuendelea kuomboleza kutokana na majukumu ya kutunza familia yaliyokuwa yanamkabili. Hivyo aliamua kurudi tena kijiweni kwake Kariakoo kuungana na jamaa zake kuendelea na shughuli zake za ukuli, Hamady alikuwa ni mtu mwenye bidii sana ya kazi na siku zote hakukubali kushindwa siku zote katika maisha yake , aliamini ugumu wa maisha ni moja ya changamoto katika maisha yangu na kuwa na imani ya kutafuta kwa juhudi kujikwamua katika hali hii ya umasikini na kumlea mama yangu vizuri, maana mimi ndiye mtoto pekee inabidi nipambane kwa uwezo wangu wote” ( Hamady aliwaza pindi anapobeba gunia la nyanya akiwa anapeleka Sokoni). Kwa kweli Hamady ni kijana anayejituma sana tena kwa uchungu kwa sababu maisha yake ni magumu na pia jicho lake likiwa linamtazama kwa mama yake kwa kuwa anampenda sana. Mungu anamsaidia Hamady kwa kumlinda wakati anaanza kazi mpaka pale anapomaliza kwa usalama. Baada ya kumaliza kazi huwa anajiandaa kwa kurudi nyumbani, kwa kawaida baada ya kazi kufanya manunuzi ya mahitaji yote ya nyumbani ndipo anachukuwa gari la Kariakoo kuelekea Kimara, wakati yupo kwenye daladala bado anaonekana mwenye mawazo sana “lini itakuwa furaha kwake kwa kuyashinda maisha haya magumu ya umaskini ili amlee mama yake? ” (alijiuliza maswali mengi wakati yupo kwenye daladala). Aliwahi kufika kituoni Kimara kwa kuwa hapakuwa na msongamano wa magari barabarani. Baada ya kuteremka kwenye daladala alijitahidi kutembea kwa haraka ili awahi kufika nyumbani kumwona mama yake kipenzi. Baada ya Hamady kuwasili nyumbani maandalizi ya chakula yakafanyika, na baada ya kumaliza kula akaelekea chumbani kwake kupumzika huku akifungulia sauti ya redio kwa mbali huku ikimuliwaza kwa muziki mzuri toka barani Ulaya uliokuwa unakonga moyo wake, Hamady alikuwa anapenda sana muziki na kuimba nyimba za wanamuziki wengi maarufu na alipenda sana kuimba nyimbo za mwanadada maarufu Celline Dion.
Itaendelea jumatatu
Kwa maoni ushauri 0712 592 790
No comments:
Post a Comment