Friday, May 20, 2016

KIBA ALAMBA DILI SONY MUSIC.

NA MWANDISHI WETU
MSANII wa Bongo Fleva nchini, Ali Kiba, jana alisaini mkataba na kampuni kubwa ya muziki ya Sony Music mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini, ambayo itakuwa inamsimamia kazi zake za muziki.
Kazi kubwa itakayokuwa ikifanya kampuni hiyo ni kusimamia video zake pamoja na audio kwa kuzilipia na kuzifikisha kwenye masoko makubwa ya muziki duniani.
Baadhi ya wasanii waliochini ya kampuni hiyo ni Davido ambaye ni msanii wa kwanza kwa Afrika wengine ni Chris Brown na John Legend.
Awali msanii huyo alikuwa na mkataba wa muda na Kampuni ya One 8 ya nchini Marekani, mbayo haikudumu ingawa aliimba wimbo na mkali wa muziki R. Kelly.


No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.