Wednesday, July 30, 2014

HUDDAH MONROE ANASWA NA UJIO MPYA WA ALI KIBA

Huddah Monroe anaswa na ujio mpya wa Ali Kiba Ujio mpya wa Ali Kiba ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wake ambao wanaoenesha kumpokea kwa mikono miwili tangu alipotambulisha nyimbo zake mbili ‘Mwana na Kimasomaso’, ingawa Mwana imeonekana kupenya zaidi. Mrembo wa Kenya aliyewahi kuwa mshiriki wa Big Brother Africa, Huddah Monroe aka The BossChick alikuwa mmoja kati ya mashabiki wa dhati walioimiss sauti ya Ali Kiba na hivi sasa wamenaswa na ujio wake mpya. Kupitia Instagram, Huddah amepost snippet ya ujio wa Ali Kiba na kuandika ujumbe unaoonesha hisia zake kwa sauti ya mwimbaji huyo. “Whaaaatttttt!!!!!!!!! I was wondering where @officialalikiba had gone to! Sauti ya kumtoa nyoka pangoni! Still my favourite Tanzanian Artist, the real definition of Bongo Flava! Duh!!” Credit:Times Fm Posted by Charles Elias Misungwi at 11:28:00 AM

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.