Monday, October 27, 2014

MARI FC WAZIDI KUJIFUA KWA NGUVU

Timu ya soka ya Mari Fc. inayoundwa na wafanyakazi wa kituo cha utafiti wa kilimo kilichopo Mikocheni jijini wiki hii iliendelea na mazoezi katika viwanja vya Changanyikeni jijini Dar ikijiandaa na michezo ya kimataifa sambamba na safari ya Zanzibar itakayofanyika baadae mwezi ujao.

Akizungumza na KAMANYANI.COM mmoja wa viongozi waandamizi wa timu hiyo Said Minazi Komba alisema timu hiyo iliyo chini ya mdhamini na mwenyekiti wa timu hiyo Dr. Joseph Ndunguru alisema ingawa michezo hiyo wanayotarajia kucheza ni ya kirafiki lakini anaamini ni muhimu sana kwa taifa na afya zao kiujumla kwakuwa inawasaidia wao kama maveterani kujikinga na magonjwa mbali mbali.


Minazi aliwataja viongozi wa timu hiyo kuwa ni Dk. Joseph Ndunguru ambaye ni mwenyekiti na mdhamini wa timu hiyo Zakaria Muyengi katibu,Masanja (Pembejeo) ambaye ni mweka hazina Dr. Juma Kayeke nidhamu na ufundi, Deo Mark nahodha wa timu, kocha Shabani Nkuliye pamoja na yeye mwenyewe Said Minazi Komba msemaji wa timu hiyo.

Minazi pia aliyataja malengo ya timu yao kuwa ni pamoja na kushiriki mabonanza mbali mbali nchini ikiwa ni sanjali na kujenga mahusiano mazuri kwa jamii na wafanyakazi kwa ujumla hususan wanamichezo.

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.