Wednesday, July 8, 2015

HADITHI

         

NA FRANCISS MAIGE


0672-249431  
 
ILIPOISHIA JUMATANO:
 Akasukuma mlango na kuingia wodini,alipo ingia ndani akakutana na Daktari mkuu akiwa na Manesi wawili wakiwa wametawaliwa na huzuni kwenye huzuni Paulo baada ya kutizama kitandani akakutana na sura ya kaka yake akiwa amelala kitandani amewekwa pamba masikioni na mdomoni kwa haraka akuweza kuamini ikabidi asogee taratibu mpaka kitandani alipolala kaka yake huku machozi ya uchungu yakiwa yanamtiririka, akamgusa kaka yake huku akiwa analia kwa uchungu sana Daktari na Manesi wakamshika Paulo na kumbembeleza na kumliwaza,baada muda mchache wakaingia Madaktari wanne wakaufunika vizuri mwili wa Mr.Ngowi na kuutoa katika...SASA SONGA NAYO


 wodi namba 16 na kuupeka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
            Daktari mkuu wa T.M.J hospital akamshika Paulo na kumtoa katika wodi ambayo alikuwepo kaka yake,wakapanda kwenye lifti wakashuka mpaka ghorofa ya pili walipo fika wakashuka na kuingia ofisini kwa Daktari mkuu aitwae Luckas kasha wakaketi lakini bado Paulo anamachunngu mengi sana baada ya kuakisha kuwa kweli aliyefariki ni kaka yake pia bado kichwa chake kinakosa majibu kila anapo tafakali alipokuwepo shemeji yake kipenzi kuwa yupo hai au amekufa……..????.Luckasi akatoa cheni ya dhahabu,saa,pete na waleti na kumkabidhi Paulo ya maana hivyo vitu ndiyo alikuwa navyo marehemu baada ya kuletwa na hospital na wasamalia wema Paulo akapokea vitu kutoka kwa Daktari na kuvishika mkononi huku akiwa ametawaliwa na mawazo mengi sana wmbayo yamekosa utatuzi kwenye kichwa chake,ndipo Daktari akaanza kumueleza Paulo kuhusu habari na shemeji yake.
“Paulo pole sana kwa matatizo maana ni sehemu ya maisha ya mwanadamu”
“asante sana Daktari nashukuru sana kwa msahada wako mungu akupe moyo uwo uwo wa imani”
“usijali ndiyo kazi yangu hiyo….ila Paulo kabla ya kukutaharifu wewe nilimpatia taarifa shemeji yako na alifanikiwa kufika hapa “
“shemeji huyu huyu mke wa Mr.Ngowi……?????”Paulo akauliza kwa mshangao huku wakitizamana na daktari.
“yap huyo huyo ndiyo alifika hapa na tukaonana na nikampatia taarifa,akuweza kuamini kabisa akapatwa na mshituko ghafla akadondoka na kupoteza fahamu ikabidi tumsaidie kwa kumpatia huduma ya kwanza lakini mpaka saa hali yake siyo nzuri kabisa”

“okay Daktari naweza kumuona shemeji yangu tafadhari naomba unisaidie kwa hilo”Paulo akawa anaomba msahada wakati machozi yanaendelea kutiririka .
“sawa twende ukamuone”
            Daktari na Paulo wakatoka nje na kuelekea wodi namba 24,walipofika wakaingia ndani Paulo akuamini kabisa alichokiona mbele ya macho kwa wakati huo baada ya kumuona shemeji yake kipenzi amelezwa akiwa anapumulia mashine ikabidi ajikaze kiume na kusogea mpaka kitandani alipokuwepo shemeji yake,akamgusa mkono na kumuita
 “shemeji ,shemeji amka,amka mimi hapa Paulo niko hapa mbele yako “Paulo akawa anamuita shemeji yake lakini akawa aamki akajaribu kumtisa lakini aikusaidia hali hiyo ilimtia wasi wasi Paulo na kuamini shemeji yako awezi kuamka tena ikabidi asogee mpaka alipokuwa Daktari na kumtaka waondoke labda siku nyingine anaweza kupata fahamu na kuweza kuamka,wakati wanataka kutoka kutoka nje kabla awajafika mlangoni wakasikia Mrs.Ngowi anakooa wakarudi kwa haraka na kumuona amefumbua mambo akaanza kulia baada tu ya kumuona Paulo na kumuuliza.
“Paulo wanangu wapo wapi……???”
“wapo nyumbani shemeji”
“nakupenda sana Paulo shemeji nakuomba uwatunze na kuwathamini wangu”
“usijali shemeji hata nakupenda”
       Baada ya kutoa usia kwa Paulo Mrs.Ngowi akafariki dunia,Paulo alihuzunika sana kwa kuwa wapoteza watu wawili wote ni muhimu katika maisha yake,ikabidi arudi nyumbani kwa ajili ya kuandaa utaratibu wa mazishi kwa kuwa mwili wa Mr.Ngowi umearibika sana kichwani kwaiyo inabidi wafanye mazishi kesho siku ya jumatano.

          Jumatano asubuhi watu wakafanya utaratibu wa kwenda kuchimba kaburi,baada ya kupata eneo katika makaburi ya kinondoni achimbaji wakachimba makaburi mawili ya Mr.ngowi na mke wake.Mnamo saa 10:15 jioni watu wakafika makabulini baada ya padre kumaliza kusoma neon kwa ajili ya kuwa takia marehemu mapumziko mema mahala pemapeponi,watoto wa Mr.Ngowi walihuzunika sana kwa kuwa poteza wazazi wao wote wawili baada ya mazishi kila mtu aliye uzulia akarudi nyumbani kwa ajili ya kuendelea na shughuli nyingine.Marafiki wengi wa Mr.Ngowi wakamtia moyo Paulo na kumtaka asiwe na hofu kila kitu kitakwenda sawa akita halibika kitu.Kila mtu aliyekuwa anafanya biashara na Mr.Ngowi alifika kutoa salamu na pole pia kutoa rambi rambi kwa kuwa wanafahamu ukarimu wa rafiki yao akuwa na ubaya na mtu na kila alikuwa mtu wa watu kwa ushauri na msahada wa kifedha akipenda kuona rafiki yake unazalilika wakati yeye yupo anaweza kikusaidia,Paulo alizidi kupata faraja kubwa moyoni mwake kwa kuona marafiki wakubwa wa kaka yake wanamfariji na kumtia nguvu katika kipindi hiki kigumu .Jioni kila rafiki wa karibu wa Mr.Ngowi akarudi kwenye makazi yake kwa ajili ya kuendelea na shughuli nyingine,ndani hoteli ya Sea cliff masaki jiji Dar es salaam kuna watu watano wanaume wane na mwanamke mmoja wakiwa wameketi ndani ya Resaurant ya Karambezi ndipo mkuu wa kikao hicho aitwae Bonny alitoa karatasi yenye mchoro wa nyumba na kuanza kuwapatia maelekezo na lengo kubwa kwenda kwenye nyumba hiyo wanayoonyeshwa wanafuata jambo moja tu ni kufanya mauaji akuna jambo jingine.Hao vijana wanne wanaume watatu na mwanadada mmoja wakakubali na kupokea kiasi cha fedha baadhi ambayo wamekubaliana na nyingine mpaka pale watakapo maliza kazi,lakini Bonny akatoa sharti moja kwa vijana waliokubali kufanya kazi yake kuwa kazi yake ifanyike ndani ya dakika 45 tu pia endapo watashindwa kupata mambo yote waliokubaliana nao ikiwemo kumuua Paulo na watoto wa Mr.Ngowi na kupata hati ya mali zote za Mr,Ngowi watapoteza maisha yao,,lakini aikuwapa hofu kabisa hao vijana kwa kuwa walishafanya kazi nyingi ngumu na zenye hatari kubwa sana na walifanikisha vyema kabisa.Baada ya kuhitimisha mazungumzo wakaondoka na kurudi kwenye makazi yao kwa ajili ya kujiandaa na majukumu mazito yanayowakabili mbele yao.  

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.