Na Ihola Mwasandube
UONGOZI
wa timu ya mpira wa wavu ya Mbozi iliyopo mkoani Mbeya, umeanza mkakati wa
kusaka vipaji katika shule za msingi
wilayani humo.
Akizungumza
na KAMANYANI.COM kwa njia ya simu jana, meneja wa timu hiyo, Callyxtus Mponzi, aliweka
wazi dhamira yao ya kusaka vipaji shuleni kuwa ni kuupa mchezo huo nafasi ya
kujulikana na jamii kirahisi kupitia wanafunzi.
"Kwa
sasa mchezo huu umeanza kupata mwamko katika wilaya ya Mbozi, tofauti na
ilivyokuwa awali, ambako tulikuwa watu wachache katika timu hii," alisema.
Mbali
na hilo, Mponzi alisema timu hiyo waliianzisha mwaka 2010, ambapo ilikuwa kama
ya mazoezi ya kujifurahisha, lakini baada ya muda wakaanza kushiriki katika
mashindano mbalimbali na hadi walipofikia kupanua wigo kuona wanafika mbali
zaidi.
No comments:
Post a Comment