Wednesday, October 22, 2014

NEW HABARI USO KWA USO NA CHUO CHA TAKWIMU IJUMAA.




Timu ya soka ya New Habari inayo milikiwa na kampuni ya New abari (2006) Limited ijumaa hii inatarajia kujitupa uwanjani kwaajili ya mtanange utakaopigika katika uwanja wa chuo cha Takwimu kilichopo Changanyikeni jijini Dar.

Mshambuliaji hatari wa New Habari Fc. Shedrack Kilasi (Hicharito) 
Akizungumza na KAMANYANI.COM mratibu wa timu hiyo Jonathan Tito alisema mchezo huo wa kirafiki unatarajia kuwa mgumu kwa upande wao kutokana na timu yake kuto fanya mazoezi kwa muda mrefu tangu walipomaliza mashindano ya Nssf mwezi wan ne hata hivyo Tito amesema kuwa timu yake itaibuka na ushindi kutokana na wachezaji wake baadhi kuwa na mazoezi binafsi na timu zao za mitaani.
Tito aliwataja baadhi ya wachezaji wanaotarajia kuanza katika kikosi chake kuwa ni pamoja na Msham Ngojwike,Kulwa Karedia,Mohamed Mharizo,Idy Suka, pamoja na msambuliaji wao tegemeo Shedrack Kilasi (Chicharito) pia alisema mechi hiyo ni mwanza tu wa mechi za kirafiki zinazotarajiwa kuwepo kila juma.

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.