Tuesday, October 7, 2014

WAZIRI APIGA STOP TFF KUTAKA KUCHUKUA 5% ZA VODACOM, AZAM TV


Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kusitisha uamuzi wake wa kutaka kuchukua asilimia 5 za udhamini wa klabu zinazotolewa na makampuni yaVodacom na Azam TV.
Nkamia ameiambia SALEHJEMBE leo kwamba ameitaka TFF kusitisha jambo hilo.
"Kweli tumekutana TFF, Bodi ya Ligi na nimeagiza suala hilo kusitishwa mara moja," alisema Nkamia.
Hata hivyo, Nkamia hakuweza kufafanua zaidi kwa kuwa alikuwa akiingia kwenye kikao.
Akaahidi kulizungumzia kwa urefu zaidi suala hilo hapo baadaye.
Nkamia atakuwa amekonga nyoyo za wadau wengi wa soka waliokuwa wameshangazwa na uamuzi wa kikatili wa TFF kutaka kuzikata klabu asilimia tano za udhamini kwa makampuni hayo mawili kwa madai fedha hizo zinapelekwa kwenye mfuko wa maendeleo ya soka.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisisitiza hakutakuwa na mjadala katika hilo na lazima klabu zikatwe fedha.
Lakini kauli ya Waziri Nkamia, aliyewahi kuwa kiongozi wa klabu ya Simba ambaye anajua ugumu wa kuendesha klabu, umesitisha alichotaka kufanya rais huyo wa TFF na kamati yake ya utendaji.

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.