Friday, May 20, 2016

DIMPOZ: YATAISHA TU



MSANII anayesifika kwa kugawa fedha kwa mashabiki wake katika baadhi ya maonyesho yake ya kimuziki, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amefunguka kuwa ipo siku tofauti zao na mkali mwenzake, Abdul Nasib ‘Diamond’ zitakwisha na watafanyakazi kama zamani.
Akizungumza juzi alipotembelea Ofisi za New Habari Limited (2006), zinazochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Rai, Dimba na The African, Ommy D alisema Diamond alikuwa rafiki yake wa karibu tangu zamani na walikuwa wakifanya kazi pamoja hivyo yaliyotokea ni moja ya mapito katika maisha ya mwanadamu yeyote.
“Siwezi kuongelea kitu chochote kinacholeta mapito haya lakini haya ni maisha nafahamu ipo siku tutakaa pamoja na kufanya kazi tena kama zamani,” alisema.


Dimpoz aliongeza kwamba kilichotokea kati yao kinaweza kutokea kwa yeyote katika maisha hivyo kinachotakiwa ni kusimama imara na kupambana na mapito hayo ndiyo maana kwa sasa kila mtu ana muziki wake na mashabiki wake.

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.