Mwamuzi, Israel Nkongo ndiye atakayelisimamia pambano la mahasimu wa soka nchini, Simba na Yanga siku ya jumapili ijayo katika uwanja wa taifa. Nkongo atakuwa ' bosi kubwa' wa mechi ya watani hao wa jadi katika soka la Tanzania, anatakiwa kuchezesha kwa kufuata sheria zote za mchezo wa soka, ni mwamuzi mwenye beji ya shirikisho la soka la kimataifa ( fifa), ila endapo atashindwa kutafsiri sheria za mchezo huo na kujikuta akifanya maamuzi mabaya, sifa yake hiyo haitakuwa na maana yoyote.
Hatakiwi ' kupiga pasi ya mwisho' kwa timu yoyote ili ipate matokeo. Anaweza kuwaziba midomo wale wote ambao wamekuwa wakimtilia shaka kuhusu kiwango chake cha uchezeshaji huku wakitolea mifano matukio yake ya nyuma, ambayo yalivuruga baadhi ya michezo. Kila mmoja anajua ukubwa wa mchezo wa Simba na Yanga, ni mechi kubwa na yenye historia ya miaka nenda rudi tangu zama za uhuru na hadi sasa inaweza kutangulia mbele ya mechi ya Gor Mahia na AFC Leopards ( mahasimu wa soka la Kenya), wakati Watanzania wakiendelea kupata radha ya Simba na Yanga kila mwaka, timu hizo za Kenya zilikuwa madaraja ya chini katika mika ya karibuni na kupandishwa kwa msaada ili kurudisha msisimko uliokuwepo
Kila mpenda soka nchini atakuwa anashikilia upande wake wakati huu, hakuna tena adhithi za timu nyingine, bali habari ni ' Simba kumfunga Yanga, au Yanga kumshinda Simba), inategemea tu na upande ambao mtu atakuwa ameangukia. Timu zote kwa kutambua uzito wa mchezo huo zimejipanga kila sehemu, sehemu muhimu ya ndani ya uwanja makocha wanajitahidi kupandisha kiwango chao cha ufundishaji, mbinu na ufundi, na bila shaka mwamuzi, Nkongo atakuwa anajifua zaidi pia ili kuongeza kiwango chake cha uchezeshaji, kama wachezaji wanaongeza nguvu na kujituma zaidi hivyohivyo pia Nkongo anavyotakiwa kufanya kwa kuwa anakwenda kucheza mechi kubwa kuliko nchini na Afrika Mashariki na Kati yote.
Tatizo kubwa la waamuzi wetu ni uoga wa kutoa maamuzi katika makosa ya awali, na atimaye mechi inapokuwa ikikolea makosa yale yanakuwa yanajirudia rudia na pale wanapoamua kuyafanyia kazi anaonekana kama anapendelea upande fulani kwa kuwa mwanzoni alishindwa kuyafanyia maamuzi kwa kuona ni makosa ya kawaida. Katika hili, Nkongo anaweza kutulia, na asiwe muoga wa kutoa maamuzi na kuyasimamia, hatakiwi kuzingirwa na kumbukumbu za matukio yaliyopita kati yake na baadhi ya wachezaji, asikubali wachezaji wamzone na endapo atawaonya na kushindwa kuheshimiwa anaweza kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria.
Katika siku za karibuni kumekuwa na madai kutoka kwa wachezaji kuwa wanajikuta wakifanya vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kuwa waamuzi pia wamekuwa wakiwatolea lugha chafu wachezaji. Ndiyo, tumekuwa tukisema kila mara kuwa mwamuzi naye ni binadamu, ila na wao wanatakiwa kutambua kuwa wachezaji pia ni binadamu hivyo endapo utawambia maneno mabaya au kumtukana anaweza kupandwa na hasira na matokeo yake kwa kuwa mwamuzi ni mkubwa kuliko mchezaji hutumia nafasi hiyo kutoa adhabu, ambayo matokeo yake inakuwa na athari kubwa kwa wengi.
Namna timu zetu zinavyokuwa zikiongozwa hasa katika mchezo huu wa mahasimu, ni ngumu sana mwamuzi kucheza pambano lao na kuonekana hukuwa na makosa, mwamuzi wa mchezo huu siku zote haaminiwi na upande wowote, na wakati inapotokea akapata nafasi ya kuaminiwa hutokea hilo kwa upande ambao umeshinda. Nasikitishwa na viwango vyetu vya kukubali matokeo, na kuna wakati unaona kabisa kuwa mwamuzi ' amepiga pasi ya mwisho pale.....' ila huna jinsi. Inawezekana Nkongo naye akawa na upande wake, kwa kuwa Simba na Yanga ndiyo zimebeba mapenzi ya kila mwanasoka nchini, kuanzia serikalini hadi mitaani kila mmoja unapofika wakati huu huonesha hisia zake za kweli kwa timu aipendayo, ila sutarajii kuona hilo kutoka kwa Nkongo. Ningependa kuona uchezeshaji wa kiwango cha juu kutoka kwake, kujiamini, kuongoza mchezo, na kufanya maamuzi kwa wakati sahihi, ni nafasi yake tena ya kung'arisha au kuchafua ' CV' yake ya uchezeshaji. Naisubiri pasi ya mwisho kutoka kwa Nkongo, niamue ' Dar es Salaam- Pacha'.

No comments:
Post a Comment