HATUA ya Nusu fainali ya michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea Mjini Khartoum nchini Sudan inatarajia kuanza kushika kasi jioni ya leo.
Mechi ya kwanza itaanza majira ya saa 11:30 jioni kwa kuwakutanisha AFC Leopard ya Kenya dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Hassan Mohamed kutoka nchini Somalia wakati mwamuzi msaidizi atakuwa ni Bogoreth Farhan kutoka nchini Djibouti.
Mechi ya pili ya nusu fainali itapigwa kaanzia majira ya saa 2:30 usiku ambapo The Victoria ya Uganda atavaana na Ahly Shandy.
Mwamuzi wa kati atakuwa ni Tadesse Belay kutoka Ethiopia na mwamuzi msaidizi atakuwa ni Bwiriza Raymond kutoka Rwanda
No comments:
Post a Comment