Thursday, June 12, 2014

SISTER P YUKO WAPI, SOMA HAPA


Anakuja ,anakuja….Sister P…..anakuja anakujaa Sister P,anakuja anakuja Sister P anakuja kwenye fani ngangariiiiiii,anakuja Sister P" ilikuwa ndo singo iliyomwingiza na kumfahamisha sokoni mwa 2002 na  ni mmoja wa wanadada wachache ambao kipindi hicho walikuw wanaendeleza mapambano katika kuhakikisha tasni ya muziki wa kizazi kipya inakwenda mbali zaidi.

Sister P, si jina geni katika tasnia ya muziki wa Kizazi Kipya hapa nchini japo amepotea kwa kitambo kirefu bila ya kusikika katika vyombo vya habari vya hapa nchini akiwa na kitu kipya.
 
Jina lake kamili ni Happiness Thadei mbali na nyimbo ya anakuja alipata kutamba na vibao kikiwemo ‘Wanachonga sana juu yangu’ Kwa sasa,‘Nani mkali’, alichomshirikisha Ney wa Mitego
na nyimbo ya  wapotezee aliyomsirikisha Dully Sykes.

Leo katika safu ya wako wapi ilimtafuta Sister P ili kuweza kuwaeleza mashabiki wake kuwa yuko wapi?na anafanya nini na ameshaachana na muziki kwani amekuwa kimya muda mrefu?

Alianza kwa kusema  kuwa pamoja na mishemishe nyingine lakini bado anafanya muziki na hataweza kuacha muziki kwani kipaji chake si cha kuiga bali amezaliwa nacho.

Aidha anasema amekuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na shughuli za kimuziki kumweka nje ya nchi. Anasema amekuwa akipiga live shows huko Burundi, Rwanda na Congo ambako alikuwa amepatiwa ofa ndefu ya kupiga shows, na anasema mpunga wake ulikuwa umenona kuweza kuiachia ofa hiyo ipite hivihivi.


Hata hivyo Sister P amesema amekuwa akinyimwa raha kwa jinsi muziki huu wa kizazi kipywa ulivyoingiliwa kwa fujo na watu wenye viwango dhoofu ambao wanauaibisha muziki huu amegundua kwamba nyimbo nyingi zinazofyatuliwa kila siku na kurushwa kwenye vyombo vya habari hazidumu kwa muda wa kutosha kwenye vyombo hivyo, jambo ambalo ni tofauti na nchi jirani ambako nyimbo nyingi haziishi utamu mapema.

Akiongelea matarajio yake ya baadae, Sister P amesema kuanza kupiga muziki wake kwa mtindo wa bendi ambao ana uhakika una maslahi zaidi kutokana na uzoefu wake alioupata nchi jirani alikokuwa akipiga mzigo

“kwa sasa nipo kimya nafanya shughuri zangu binafsi za jamii na sio kwamba nimeachana na muziki,ila siku nikitaka kurudi kwenye game nitakuwa naimba kwa mtindo wa bendi ambao ana uhakika una maslai





zaidi kutikana na uzoefu wangu nilioupata nchi jirani”alisema Sister P

Aidha Sister P anasema hatoweza kusahau katika maisha yake alipoharibikiwa mimba wakati akiwa anafanya mazoezi makali ya kukimbia ufukweni pamoja na kiungia Gym ili apate stamina ya kupasuka vizuri kwenye ‘mic’kumbe alikuwa anauweka rehani ujauzito wake

“Nilikuwa nafanya mazoezi makali ya kukimbia ufukweni pamoja na kuingia gym ili nipate stamina ya kupasuka vizuri kwenye ‘mic’ kumbe nilikuwa nauweka rehani ujauzito wangu
 
“Siku moja baada ya kutoka mazoezini nikaenda studio kuingiza sauti, wakati naendelea
kufanya makamuzi nikapatwa na maumivu makali tumboni nikkimbizwa Hospitalini na baada ya uchunguzi ikagundulika kuwa mimba imeharibika”alisema Sister P



No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.