Rehema akikubali kuolewa na Chaz.
Wakikumbatiana baada ya kufunga ndoa.
Chaz Baba akimpigia simu bi harusi (mkewe) ili awahi misa ya ndoa yao. Bw. na Bi Deo Mutta waliokuwa wasimamizi wa Chaz Baba.
Chaz Baba (kulia) akiwa na marafiki zake.
Bi harusi, Rehema, kabla hajashuka.
Bi harausi akiwekwa sawa kuingia kanisani.
Chaz na Rehema wakielekea kanisani kufunga ndoa.
Chaz na mkewe wakifuatilia misa ya ndoa yao.
Mchungaji wa kanisa hilo akitoa somo la ndoa.
Maharusi wakiwa wamepiga magoti.
…Wakifungishwa ndoa.
Wakitoka kanisani.
Wakionyesha vyeti vyao.
RAIS wa bendi ya Mashujaa, Charles
Gabriel Cyprian ‘Chaz Baba’, juzikati aliua ndege wawili kwa wakati
mmoja pale alipotoa burudani ya nguvu katika sherehe ya harusi yake
iliyofanyika katika ukumbi wa Mirado Hall uliopo Sinza Makaburini jijini
Dar, na pia kutinga katika ukumbi wa Mango Gadern Kinondoni jijini Dar
ambapo Twanga Pepeta walikuwa wakiendeleza wimbi la burudani katika
ukumbi huo.Tukio hilo la Chaz kutinga katika ukumbi wa Mango liliwashangaza wengi kwani kwa wakati ule Chaz alitakiwa kwenda kupumzika kutokana na mkewe kuonekana amechoka kwa sababu ya ujauzito wake.
“Shemeji yetu anaonekana kachoka sana lakini Chaz ndio kwanza anaonekana hana hata muda wa kwenda kulala mapema” alisema shabiki mmoja aliyekuwa ndani ya ukumbi.
Chaz Baba alifunga ndoa na Rehema Sospeter Marwa, siku ya Agosti 24, mwaka huu katika kanisa la St Peters jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment