Wednesday, August 28, 2013

RAY C SASA AINGIA GYM RASMI.

ray c 
Zaidi ya sauti yake na uwezo mkubwa wa kuimba nyimbo zinazoshikika kiurahisi, umaarufu wake mwingine mkubwa toka enzi hizo ni kiuno bila mfupa kwa jinsi alivyokua akicheza nacho….. ni uwezo uliofanya mpaka maneno ya kiuno bila mfupa yakapata umaarufu kupitia yeye.
 
Siku kadhaa tu baada ya kutangaza kurudi kwenye muziki kama zamani, Ray C akiwa ametoka kwenye matibabu ya matumizi ya dawa za kulevya… ameanza kujipanga kupunguza unene alionao ili awe mwepesi zaidi ya alivyo sasa ili kila kitu kiende kama kilivyokua.
 
Ray C akipiga story na fans wake alisema “Mauno ni nyonga si manyama”, hii ni moja ya sababu za msingi sana zilizomfanya Rehema Chalamila kuingia gym kuanza mazoezi.
ray4 ray3 ray2

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.