Monday, October 28, 2013

BENZI LA MADAM RITTA WA BSS LAUNGUA MOTO

Gari aina ya Benzi iliyokuwa ikimilikiwa na mkurugenzi wa Benchmark production Madame Rita Juzi iliwaka moto ghafla na kuungua vibaya.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea maeneo ya Chuo kikuu cha mlimani sehemu ya Udasa, akizungumza kwa masikitiko makubwa dereva wa gari gilo aliyefahamika kwa jina la Julius alisema gari hilo lilizima ghafla na milango ikajiloki lakini baada ya jitihada za kuliwasha liliwaka tena ndipo alipotaka kuendelea na safari lakini baada ya mita kama kumi gari lilianza kuunguruma kwa tabu ndipo aliteremka kwa ajili ya kufunua boneti lakini alipofanikiwa kufanya hivyo tu akasikia mlipuko mkubwa wa betri ya gari hilo na kisha kufuatiwa na moto mkubwa ulioliunguza gari zima.

Julius anasema katika tukio hilo hakufanikiwa kuokoa kitu chochotye zaidi ya maisha yake. "Dah! acha tu kaka, yaani ilikuwa kama movie vile, ila namshukuru Mungu tu nilichomoka salama ingawa nililazwa hospitali ile juzi baada ya ajali kwakuwa nilikuwa na presha, si unajua mali za watu hizi." Alisema julius.

KAMANYANI.COM ilijitahidi kumtafuta Chifu jaji wa Bss ili kudodosa zaidi kutokana na tukio hilo lakini simu yake haikuwa hewani hata hivyo tunampa pole dereva na mmiliki wa ndinga hiyo yenye thamani ya Tsh, 80 mil.


No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.