Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani kwa marehemu Julius Nyaisangah eneo la Kihonda Mtaa wa Viwandani mkoani Morogoro.
MAREHEMU Julius Nyaisangah 'Uncle J'
amefariki dunia siku ya jana asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu. Akizungumza
na Mtandao huu, Mke wa marehemu, Leah Nyaisangah amesema kuwa mumewe
alilkuwa akisumbuliwa na magonjwa ya sukari na shinikizo la damu kwa
muda mrefu na amefariki leo asubuhi. Marehemu Nyaisangah mpaka mauti
yanamfika alikuwa Meneja Mkuu wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro.
Marehemu ameacha mke na watoto watatu ambao ni Samwel, Noela na
Beatrice. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwa mazishi
yatakayofanyika nyumbani kwao Tarime.
No comments:
Post a Comment