
Akizungumza na blog hii mkali huyo alisema ngoma hiyo ameshaanza kuisambaza kwenye vituo mbali mbali vya redio na anamshukuru Mungu ngoma imeanza kupigwa angarau mara kadhaa kwa siku na kumfanya ajipange zaidi na kujizatiti il kuhakikisha anafyatua chombo kingine siku si nyingi. "Ndiyo kaka, namshukuru Mungu Ma Dj hawajanibania sana kwani kwenye vituo mbali mbali vya redio ngoma imekuwa ikichezwa kinoma na hii imekuwa ni changamoto kwangu kuhakikisha nafanya ngoma nyingine siku si nyingi ili kuzidi kukonga nyoyo za masabiki wangu." Alisema msanii huyo.
Hata hivyo Taacici wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi alikuwa akijiandaa kwenda mjini Makambako wilayani Njombe ambako alisema kulikuwa na show moja aliyokuwa akitegemea kuipiga kwenye tamasha moja lilikuwa linaandaliwa na kituo cha Redio moja kilichopo mjini Iringa alisema alikuwa akiisikilizia simu ya meneja mmoja ambaye ilikuwa wakubaliane kuhusu malipo ya show hiyo na siku chache baadae angeondoka kuelekea mjini humo.
Akizungumza kwa furaha kutokana na kuonekana kupokelewa kwa mikono miwili na mashabiki wa Bongo flavor Taacici alisema amejipanga vyema kuhakikisha kila anapopata nafasi ya kupanda Jukwaani anahakikisha anafanya kazi ya uhakika ili kujiongezea mashabiki lukuki na kuwafunika baadhi ya wasanii wenye maringo kwa mashabiki huku akisisitiza kwamba hata siku moja hata dhubutu kuleta maringo kwa mashabiki wake kwani ndio mtaji kwake.
Taacici pia aliwaasa Madj kadhaa ambao wamekuwa wakiomba hongo ili kupiga nyimbo za wasanii akisema kufanya hivyo si kuusaidia muziki wa kizazi kipya lakini akawasifia wengine ambao wamekuwa wakiigonga kwa fujo ngoma yake huku akiwa hana kitu na hajawapa fedha yoyote. "Unafikiri kaka, kuna watu nimewapa cd kama cd sijawapa mpunga wala nini lakini ngoma mpaka kesho inagongwa mwanzo mwisho, lakini kuna wengine wana majigambo na maringo meeengi ili msanii uwape mshiko ndipo wagonge ngoma yako, sasa kama mtu una malengo ya kuwa msanii wa kimataifa halafu watu wa hapa home wanakuangusha unadhani utatoka lini?" Alisema Taacici.
Mkurugenzi wa blog hii anamtakia kila lakheri msanii huyo na wengine wenye juhudi kama zake.
Kuisikiliza ngoma hii bonyeza chini..
No comments:
Post a Comment