Friday, April 1, 2016

AJALI MBAYA YATOKEA CHUO KIKUU CHA DAR LEO.

Ajali mbaya imetokea maeneo ya Chuo kikuu cha Dar es salaam mapema leo katika eneo la majumba 20 barabara ya Changanyikeni.
Katika ajali hiyo ambayo imehusisha gari moja lililo pinduka baada ya kupaa juu kwa umbali wa mita nne na kwenda urefu wa mita arobaini hakuna aliye fariki lakini watu wawili waliokuwa ndani ya gari waliumia vibaya na kukimbizwa hospitali, mpaka tunaondoka  eneo la tukio askari wa doria chuoni hapo na wakazi wa maeneo ya karibu na chuo walikuwa wakiendelea kushangaa.
Baadhi ya mashuhuda walioliona tukio la ajali hiyo wanasema chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa gari hilo ambaye baada ya kona kumshinda ndipo gari likapaa na kuingia bondeni. 






No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.