Monday, May 16, 2016

KILA JUMATATU MWANANGU MWENYEWE:




























FID FID Q VS AFANDE SELE

Kama nawadeku hivi kiaina masela wangu, leo sina ngenga kiviiiile lakini kama kawa nawasongeshea wakali wawili ambao pia kwa namna nyingine naweza kusema wote ni wakongwe hapa namzungumzia Fid Q mkali kutoka Mwanza na Afande Sele kutoka Moro yaani mji kasoro bahari, Utata upoje, shuka nah ii.
Msela Fid Q aligonga ngoma kali aliyoisongesha kwa jina la Mwanza ngoma hii mbali na kumwongezea mashabiki lukuki lakini pia ilimuweka pazuri kwenye gemu nakumfanya apige salari kibao kupitia shoo zake, unan’soma mwanangu, basi msela ndani ya ngoma hiyo akatupia mistari inayosema.
  “ Wewe ukipata mia sifuri atapewa nani wengi hufyata wakisikia nimenata na biti za Majani walishanitabiri watu wangu wa mtaani, mi ndiye mfalme atayefuata baada ya Selemani.” Inasikika mistari hiyo.
Ukawa mchana ikawa usiku Afande naye akaingia zake chimbo na kunyonga bonge la biti ambalo ndani yake alisukuma ngoma aliyoisongesha kwa jina la Karata dume akisimama na msela mwingine Dk.Levy ndani ya ngoma hii akatupia mistari iliyoonekana kama ni jibu kwa mistari hii inasema.
 “Simtazame mwingine kumpa mikuki na sime,hata nikimtazama siseme mpaka nimpime, anaweza kurithi ufalme  ama anataka ujiko aonekane ndiyo kidume na kisha akamate mshiko wake za watu wamkome  kinyume na mimi Mfalme.”
Oya masela, mimi acha niingie zangu kitaa kuisaka mistari mingine jumatatu tugumiane hapa wanangu wenyewe, dadadadek!


No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.