Timu ya soka ya Uvc inayoundwa na wafanyakazi na maprofesa kutoka chuo kikuu na maeneo ya jirani leo asubuhi imekubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa maveterani wenzao wa Kikunguni Veterani wenye maskani yao Gongolamboto katika mtanange wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Chuo kikuu cha mlimani.
Wakicheza kwa kasi na kujiamini Kikunguni walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Babu Ally dakika ya 12 ambaye alifumua shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Uvc Mohamed Makongo.
Hata hivyo Uvc walijikakamua na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Jumanne Ombopa ambaye alipiga shuti akiwa umbali wa mita 40 na kiandikia Uvc bao la kusawazisha.
Matokeo hayo yalidumu hadi kipindi cha pili ambapo kila timu ilifanya mabadiliko huku Uvc wakimtoa Shedrack Kilasi na nafasi yake kuchukuliwa na Rajabu Said na Kikunguni wakamtoa Babu Ally na nafasi yake kuchukuliwa na Hemed Godfrey.
Hata hivyo mabadiliko hayo yalikuwa na manufaa kwa Kikunguni Veterani kwani dakika ya 80 Hemed Godfrey aliyeingia kutoka benchi aliifungia timu yake bao la pili na la ushindi hivyo mpaka mtanange unamalizika ngoma ilikuwa nyali nyali.
Kesho jumapili timu hiyo ya UVC itashuka dimbani hapo kufanya mazoezi kama kawaida yao.
No comments:
Post a Comment