Thursday, August 29, 2013

TFF YAWAJIBU YANGA

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa amesema kamati yake haikumhoji winga wa Yanga, Mrisho Ngassa ilijitosheleza na maelezo ya kimaandishi.
 
Ngasa amefungiwa kucheza mechi sita za mashindano na kutakiwa kuilipa Simba kiasi cha Sh45 milioni kufuatia kubainika kusajili mikataba ya klabu mbili kwa wakati mmoja.
 
Klabu yake ya Yanga imekata rufaa kupinga uamuzi huo, ambapo pamoja namambo mengine inaona mchezaji wake hakupewa haki ya kujieleza kufuatia tuhuma alizokuwa akikabiliwa nazo.
 
Lakini jana wakati Mwenyekiti, Mgongolwa akizungumza na gazeti hili alisema kamati yake inafanya kazi na vielelezo vya maandishi, hivyo hawakuona sababu ya kumwita Ngasa.
 
“Kimsingi, watu wanatakiwa kufahamu, sisi kama kamati tunatumia maelezo ya maandishi ambayo ndio vithibitishoi vyetu, na kama ushahidi wa vielelezo utakuwa na upungufu ndipo tunapomwita mchezaji,” alisema Mgongolwa. Akifafanua alisema: “Kuna wachezaji wengi usajili wao umeonekana kuwa na matatizo, lakini hatukuwai kuwahoji.”

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.