Wasanii hao waliwashangaza watu jinsi walivyokuwa wakijituma kukata
mauno huku Wolper akimtunza mpiga ngoma na kumkatikia kwa staili
mbalimbali zikiwemo za chumbani.
“Yaani wewe ulikosa mambo, Snura alitoa shoo na mapacha wake
utadhani alikuwa amelipwa, yaani walinogesha ngoma ya kumuaga mdogo wake
Vanitha ambaye anakwenda kufunga ndoa Dodoma,” alisema sosi aliyekuwa
akimsimulia mwandishi wetu.
Aidha, wageni waliokuwa wamealikwa eneo hilo hawakudhani kama Wolper
na Aunt wangeweza kujituma vile kama walivyokuwa wakikata mauno hayo kwa
sababu ustaa wote waliuweka pembeni na kujiachia kwa raha zao.
No comments:
Post a Comment