KOCHA `mbwatukaji` Jose Mourinho amekiri kuwa Chelsea inavutiwa kumsajili Cesc Fabregas kutoka klabu ya FC Barcelona, huku mchezaji mwenzake wa Hispania Gerard Pique amesema dili hilo limekamilika kwa paundi milioni 26.8
Kocha huyo amesema kuwa ni wazi Fabregas anataka kurudi ligi kuu ikiwa ni miaka mitatu imepita tangu aondoke Asernal, hivyo anafuatilia kwa makini ili kumsajili baada ya kombe la dunia.
Wakati huo huo Chelsea wako tayari kumpa ofa ya mshahara wa paundi milioni laki mbili kwa wiki winga wao hatari, Eden Hazard ili kuwaziba mdomo Paris Saint-Germain wanaoiwinda saini yake.
“Kuna mchakato huko anakotaka kuondoka, anataka kuja England kwasababu ni taifa analopenda kucheza. Tunavutiwa kufuatilia hali halisi”.
Wakati huo huo, Pique kwa upande wake anasema dili hilo limekalimika. Beki huyo wa Hispania alinaswa na Kamera mjini Washington akimwambia kocha wa Hispania , Vicente del Bosque kuwa Fabregas ataondoka Barcelona kwa dau la paundi milioni 26.8 baada ya klabu hiyo kumalizia msimu bila kikombe.
Gerard Pique alinaswa na kamera akimwambia kocha wa Hispani Vicente del Bosque kuhusu kuondoka kwa Fabregas.
No comments:
Post a Comment