Thursday, July 3, 2014

SHABANI KONDO KUKIPIGA DARAJA LA TATU

Kuna kila dalili za mchezaji aliyetemwa na Yanga kukipiga kwenye timu ya Changanyikeni rangers inayoshiriki ligi daraja la tatu mkoa wa Dar, kwani tangu timu hiyo ilipoingia kambini kujiandaa na ligi hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi ujao staika huyo amekuwa akihudhuria mazoezi ya timu hiyo ya matajiri wa Changanyikeni. "Tulimsajili Moses Godwin kutoka simba nahisi mfadhili anataka kumsajili na huyu jamaa ili atupige tafu." Alisikika shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Peter aliyekuwa akifuatilia mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye uwanja wa chuo cha Takwimu Changanyikeni.

 Kondo wa tatu akibadili nguo baada ya mazoezi kumalizika


No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.