Tuesday, September 9, 2014

CHEKI PICHA CHANGANYIKENI RANGERS ILIVYO ISASAMBUA TP 1-0

siku ya jumapili ilikuwa tamu kwa chama tishio wilaya ya Kinondoni la Changanyikeni Rangers ambalo pia hivi majuzi kati tu lipanda daraja na sasa litakipiga ligi daraja la pili. Chama hili tishio linalonolewa na wakongwe wa zamani Kamba Lufo na Steven Nyenge jumapili liliitia adabu timu dhaifu ya Tip yenye maskani yake Sinza katika mchezo wa ligi ya Ujenzi uliochezwa katika uwanja wa Kinesi uliopo maeneo ya Shekilango Ubungo, bao la Changanyikeni lilifungwa na Issa Shaibu kwa shuti kali na mpaka mtanange unamalizika matokeo yalikuwa ni Changanyikeni 1-0 Tip. Timu hizo zitarudiana tena Kesho alhamisi ili kumtafuta mshindi atakaye songa mbele katika ligi hiyo ya ujenzi ambayo inachezwa kwa mtindo wa mtoano nyumbani na ugenini.

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.