Monday, June 15, 2015
AJARI MBAYA YATOKEA IRINGA
Watu zaidi ya 10 wamepoteza maisha usiku huu katika ajali ya gari aina ya costa mali ya Another G inayofanya safari zake kati ya Njombe - Iringa baada ya kugongana na Lori/Semi Trailler
Taarifa za awali ambazo tumezipata kutoka eneo la tukio zinadai kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Kinyanambo nje kidogo na mji wa Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakati gari hiyo ya Another G ikitokea Njombe kwenda Iringa.
Mbali ya kuwa maiti ambazo zimetolewa na kufikishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya wilaya ya Mufindi kuwa zimekwisha fika zaidi ya 10 ila inadai kuwa idadi ya miili inaweza kuongezeka zaidi kutokana na kazi ya uokoaji ikiendelea eneo la tukio.
UPDATES:
Inaelezwa kuwa waliofariki dunia mpaka sasa ni 22 wanaume 15 na wanawake 7 na majeruhi ni 34.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Anakuja ,anakuja….Sister P…..anakuja anakujaa Sister P,anakuja anakuja Sister P anakuja kwenye fani ngangariiiiiii, anakuja Sister P...
-
Hii ilitokea jana kwenye viwanja vya Reders club ambapo wahudumu wa Castle Lager waliokuwa wakihudumia wakati tamasha Bonanza la kuwasaka wa...
No comments:
Post a Comment