ILIPOISHIA JUMATANO:
“naongea na nani mwenzangu…….???”mdogo
wake Mr.Ngowi aitwaye Paulo akauliza
“unaongea na Daktari mkuu kutokea T.M.J
hospital”daktari akajibu
Ikabidi Paulo anyanyuke aliko kuwa
ameketi na kusogea pembeni kidogo kwa lengo la kuzungumza vizuri na Daktari.
SASA ENDELEA
“okay nakusikiliza “
“sisi wanaume tumepewa moyo wa uvumilivu
kwa kila jambo,kitu ninacho kwambia naomba ujikaze kama mwaume sawa…..??”Daktari
akamuuliza Paulo kama anaweza kuvumilia kupokea ujumbe mzito kuhusu kifo cha
kaka yake.
“sawa nakuhaidi nitavumilia”Paulo
akajibu akiwa amejawa na hofu kubwa moyoni mwake pia kichwa kikiwa kimejawa na
maswali mengi yaliyo kosa majibu kwa muda mchache.
“kaka yako Mr.ngowi ametutoka atunaye
tena dunia kuanzia sasa pole sana ndugu yangu”
“sawa nimekuelewa “Paulo akajibu kwa
unyonge huku machozi yakiwa yanamtiririka.
“pole sana nakuomba ufike hapa hospital
hili uchukue baadhi ya vitu vya muhimu alivyo kuwa acha marehemu”Daktari baada
ya kusitisha mazungumzo Paulo aligundua taarifa hiyo ya kifo cha kaka yake
imemuhuzunisha sana, akutaka kabisa kumueleza taarifa nyingine ya huzuni kuhusu
shemeji yake mke wa Mr.Ngowi mpaka pale atakapofika hospital.
“okay Daktari hiyo hospitali ya T.M.J
iko sehemu hapa Dar es salaam……..??”Paulo akamuuliza Daktari hili amuelekeze
.Jmaana akuwa anapafahamu T.M.J hospital.
“sawa T.M.J hospital ipo mikocheni Kawawa
road,inatazamana na Mayfair Plaza”Daktari akamjibu “okay Daktari hiyo hospitali
ya T.M.J iko sehemu hapa Dar es salaam……..??”Paulo akamuuliza Daktari hili
amuelekeze maana akuwa anapafahamu T.M.J hospital.
Paulo aliumia sana baada ya kupata
taarifa ya kifo cha kaka yake aliyekuwa anamtegemea kwa msahada mkubwa,alishindwa
kuamini asilimia mia mpaka pale atakapo fika hospital na kuuona mwili wa kaka
yake, kwa kuwa muda wa masaa matatu yaliyo pita walikuwa pamoja maeneo
wakijadili mambo ya kukuza kampuni zao mpya walizo fungua hili wapate faida
nzuri ikiwezekana miaka kazaa ijayo wawe na miladi nje ya mipaka ya Tanzania
nchi jirani kama Malawi,Zimbabwe,Uganda na Kenya lakini mipango ya mungu aina
makosa maana sisi tunapanga Mungu utimiza aina namna tushukuru kwa yote ndiyo
kauli aliyo jifaliji nayo Paulo akatoa simu yake ya kiganjani aliyoweka kwenye
mfuko wa shati na kutafuta namba ya shemeji yake mke wa Mr.Ngowi baada ya
kuipata akampigia lakini ikawa haipatikani.Paulo alizidi kuchanganikiwa ikabidi
atoke nje na kutuacha sisi tunacheza game ya magari iitwayo play station, bila
kutambua chochote kinachoendelea kuhusu wazazi wetu.Baada ya Paulo kutoka nje
akamuita mlinzi na kumueleza kila kitu kinachoendelea kuhusu kifo cha Mr.Ngowi
lakini Paulo akataka mlinzi aonyeshe hali yoyote hili watoto wasielewe
kinachoendelea mpaka pale watapokuwa wamefika hospital na kupata uwakika.mlinzi
aitwae John akafungua geti,ikabidi Paulo aingie ndani ya gari na kuelekea
hospital bila ya kutuaga kwa kuwa akutaka sisi tufahamu chochote
kinachoendelea,kila wakati Paulo alipokuwa anaendesha gari akajaribu kumpigia
shemeji yake katika simu yake ya kiganjani lakini akufanikiwa kumpata kabisa
alizidi kupatwa na hofu zaidi,kwa kuwa barabarani hapakuwa na msongamano wa
gari kabisa ikasadia Paulo kufika kwa haraka hospital akapaki gari vizuri
akashuka na kuingia hospital kabla ya kumpigia Daktari aliyempatia taarifa ya
kifo cha kaka akampigia tena shemeji yake lakini bado simu yake ya kiganjani
ikawa haipatikani, Paulo akampigia Daktari mkuu aliyempatia taarifa simu ikaita
kwa muda na kupokelewa.
“helooo…Daktari nimeshafika hapa T.M.J
hospital”
“okay uko wapi”Daktari akamuuliza Paulo.
“nipo hapa mapokezi “Paulo akajibu
“okay panda lifti njoo ghorofa ya tatu
wodi namba 16”
“sawa Daktari nakuja”
Paulo akasogea hatua chache kutoka
pale alipo kuwa mpaka palipokuwa na lifti,akabonya kitufe kati ya vitatu
vilivyokuwa na alama tofauti tofauti atimaye lifti ikafunguka na Paulo akaingia
ndani na kuelekea ghorofa ya tatu,baada ya kufika akatoka kwenye lifti na
kuanza kutizama avijibao vidogo vidogo vilivyo kuwa kwenye kila wodi na
kuandika namba za wodi,macho ya Paulo yalitizama huku na kule mwishowe
akakutana na wodi namba16.
Akasukuma mlango na kuingia wodini,alipo ingia ndani akakutana na
Daktari mkuu akiwa na Manesi wawili wakiwa wametawaliwa na huzuni kwenye huzuni
Paulo baada ya kutizama kitandani akakutana na sura ya kaka yake akiwa amelala
kitandani amewekwa pamba masikioni na mdomoni kwa haraka akuweza kuamini
ikabidi asogee taratibu mpaka kitandani alipolala kaka yake huku machozi ya
uchungu yakiwa yanamtiririka, akamgusa kaka yake huku akiwa analia kwa uchungu
sana Daktari na Manesi wakamshika Paulo na kumbembeleza na kumliwaza,baada muda
mchache wakaingia Madaktari wanne wakaufunika vizuri mwili wa Mr.Ngowi na
kuutoa katika ITAENDELEA JUMATANO
No comments:
Post a Comment