NA FRANCISS MAIGE
0672-249431
ILIPOISHIA JUMATANO:
Akasukuma mlango na kuingia wodini,alipo ingia ndani akakutana na Daktari mkuu akiwa na Manesi wawili wakiwa wametawaliwa na huzuni kwenye huzuni Paulo baada ya kutizama kitandani akakutana na sura ya kaka yake akiwa amelala kitandani amewekwa pamba masikioni na mdomoni kwa haraka akuweza kuamini ikabidi asogee taratibu mpaka kitandani alipolala kaka yake huku machozi ya uchungu yakiwa yanamtiririka, akamgusa kaka yake huku akiwa analia kwa uchungu sana Daktari na Manesi wakamshika Paulo na kumbembeleza na kumliwaza,baada muda mchache wakaingia Madaktari wanne wakaufunika vizuri mwili wa Mr.Ngowi na kuutoa katika...SASA SONGA NAYO
wodi namba 16 na kuupeka kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti.
Daktari mkuu wa T.M.J hospital
akamshika Paulo na kumtoa katika wodi ambayo alikuwepo kaka yake,wakapanda
kwenye lifti wakashuka mpaka ghorofa ya pili walipo fika wakashuka na kuingia
ofisini kwa Daktari mkuu aitwae Luckas kasha wakaketi lakini bado Paulo
anamachunngu mengi sana baada ya kuakisha kuwa kweli aliyefariki ni kaka yake
pia bado kichwa chake kinakosa majibu kila anapo tafakali alipokuwepo shemeji
yake kipenzi kuwa yupo hai au amekufa……..????.Luckasi akatoa cheni ya
dhahabu,saa,pete na waleti na kumkabidhi Paulo ya maana hivyo vitu ndiyo
alikuwa navyo marehemu baada ya kuletwa na hospital na wasamalia wema Paulo
akapokea vitu kutoka kwa Daktari na kuvishika mkononi huku akiwa ametawaliwa na
mawazo mengi sana wmbayo yamekosa utatuzi kwenye kichwa chake,ndipo Daktari
akaanza kumueleza Paulo kuhusu habari na shemeji yake.
“Paulo pole sana kwa matatizo maana ni
sehemu ya maisha ya mwanadamu”
“asante sana Daktari nashukuru sana kwa
msahada wako mungu akupe moyo uwo uwo wa imani”
“usijali ndiyo kazi yangu hiyo….ila
Paulo kabla ya kukutaharifu wewe nilimpatia taarifa shemeji yako na alifanikiwa
kufika hapa “
“shemeji huyu huyu mke wa Mr.Ngowi……?????”Paulo
akauliza kwa mshangao huku wakitizamana na daktari.
“yap huyo huyo ndiyo alifika hapa na
tukaonana na nikampatia taarifa,akuweza kuamini kabisa akapatwa na mshituko
ghafla akadondoka na kupoteza fahamu ikabidi tumsaidie kwa kumpatia huduma ya
kwanza lakini mpaka saa hali yake siyo nzuri kabisa”
“okay Daktari naweza kumuona shemeji
yangu tafadhari naomba unisaidie kwa hilo”Paulo akawa anaomba msahada wakati
machozi yanaendelea kutiririka .
“sawa twende ukamuone”
Daktari na Paulo wakatoka nje na
kuelekea wodi namba 24,walipofika wakaingia ndani Paulo akuamini kabisa
alichokiona mbele ya macho kwa wakati huo baada ya kumuona shemeji yake kipenzi
amelezwa akiwa anapumulia mashine ikabidi ajikaze kiume na kusogea mpaka
kitandani alipokuwepo shemeji yake,akamgusa mkono na kumuita
“shemeji ,shemeji amka,amka mimi hapa Paulo
niko hapa mbele yako “Paulo akawa anamuita shemeji yake lakini akawa aamki
akajaribu kumtisa lakini aikusaidia hali hiyo ilimtia wasi wasi Paulo na
kuamini shemeji yako awezi kuamka tena ikabidi asogee mpaka alipokuwa Daktari
na kumtaka waondoke labda siku nyingine anaweza kupata fahamu na kuweza
kuamka,wakati wanataka kutoka kutoka nje kabla awajafika mlangoni wakasikia
Mrs.Ngowi anakooa wakarudi kwa haraka na kumuona amefumbua mambo akaanza kulia
baada tu ya kumuona Paulo na kumuuliza.
“Paulo wanangu wapo wapi……???”
“wapo nyumbani shemeji”
“nakupenda sana Paulo shemeji nakuomba
uwatunze na kuwathamini wangu”
“usijali shemeji hata nakupenda”
Baada ya kutoa usia kwa Paulo Mrs.Ngowi
akafariki dunia,Paulo alihuzunika sana kwa kuwa wapoteza watu wawili wote ni
muhimu katika maisha yake,ikabidi arudi nyumbani kwa ajili ya kuandaa utaratibu
wa mazishi kwa kuwa mwili wa Mr.Ngowi umearibika sana kichwani kwaiyo inabidi
wafanye mazishi kesho siku ya jumatano.
Jumatano asubuhi watu wakafanya
utaratibu wa kwenda kuchimba kaburi,baada ya kupata eneo katika makaburi ya
kinondoni achimbaji wakachimba makaburi mawili ya Mr.ngowi na mke wake.Mnamo
saa 10:15 jioni watu wakafika makabulini baada ya padre kumaliza kusoma neon
kwa ajili ya kuwa takia marehemu mapumziko mema mahala pemapeponi,watoto wa
Mr.Ngowi walihuzunika sana kwa kuwa poteza wazazi wao wote wawili baada ya
mazishi kila mtu aliye uzulia akarudi nyumbani kwa ajili ya kuendelea na
shughuli nyingine.Marafiki wengi wa Mr.Ngowi wakamtia moyo Paulo na kumtaka
asiwe na hofu kila kitu kitakwenda sawa akita halibika kitu.Kila mtu aliyekuwa
anafanya biashara na Mr.Ngowi alifika kutoa salamu na pole pia kutoa rambi
rambi kwa kuwa wanafahamu ukarimu wa rafiki yao akuwa na ubaya na mtu na kila
alikuwa mtu wa watu kwa ushauri na msahada wa kifedha akipenda kuona rafiki
yake unazalilika wakati yeye yupo anaweza kikusaidia,Paulo alizidi kupata
faraja kubwa moyoni mwake kwa kuona marafiki wakubwa wa kaka yake wanamfariji
na kumtia nguvu katika kipindi hiki kigumu .Jioni kila rafiki wa karibu wa
Mr.Ngowi akarudi kwenye makazi yake kwa ajili ya kuendelea na shughuli
nyingine,ndani hoteli ya Sea cliff masaki jiji Dar es salaam kuna watu watano
wanaume wane na mwanamke mmoja wakiwa wameketi ndani ya Resaurant ya Karambezi ndipo
mkuu wa kikao hicho aitwae Bonny alitoa karatasi yenye mchoro wa nyumba na
kuanza kuwapatia maelekezo na lengo kubwa kwenda kwenye nyumba hiyo wanayoonyeshwa
wanafuata jambo moja tu ni kufanya mauaji akuna jambo jingine.Hao vijana wanne
wanaume watatu na mwanadada mmoja wakakubali na kupokea kiasi cha fedha baadhi
ambayo wamekubaliana na nyingine mpaka pale watakapo maliza kazi,lakini Bonny
akatoa sharti moja kwa vijana waliokubali kufanya kazi yake kuwa kazi yake
ifanyike ndani ya dakika 45 tu pia endapo watashindwa kupata mambo yote
waliokubaliana nao ikiwemo kumuua Paulo na watoto wa Mr.Ngowi na kupata hati ya
mali zote za Mr,Ngowi watapoteza maisha yao,,lakini aikuwapa hofu kabisa hao
vijana kwa kuwa walishafanya kazi nyingi ngumu na zenye hatari kubwa sana na
walifanikisha vyema kabisa.Baada ya kuhitimisha mazungumzo wakaondoka na kurudi
kwenye makazi yao kwa ajili ya kujiandaa na majukumu mazito yanayowakabili
mbele yao.
No comments:
Post a Comment