Wednesday, November 18, 2015

AUNT EZEKIEL MWANANGU HAJAFANANA NA NYALANDU



Msanii wa filamu ambaye hivi karibuni amejipatia hadhi ya kuitwa mama, Aunt Ezekiel amewashushua wanaosambaza taarifa kuwa mwanaye amefanana sura na kigogo mmoja mkubwa serikalini ndiyo maana anamficha sura yake kwa kuwa watu watamjua.
Akipiga stori na waandishi wetu, Aunt Ezekiel alisema kuwa huo ni uongo mtupu na kuongeza kuwa kuna watu wengine wa karibu walidai mwanaye ni Mhindi lakini wameumbuka wenyewe baada ya kumwona.
Aunt aliweka kinaga ubaga kuwa mtoto wake hajafanana na Nyarandu na ndiyo maana mpaka leo yupo na mpenzi wake Iyobo kwa kuwa mtoto huyo angefanana na kigogo yeyote kama inavyodaiwa basi wangegombana na Iyobo mara tu alipozaliwa mtoto huyo.
“Cookie siyo Mhindi wala hajafanana na Nyalandu, ni Mbongo ‘pyua’ kama mimi na Iyobo, sasa sijui hao watu mambo mengine wanayatolea wapi, kikubwa wasubiri ipo siku nitamwonesha na kumweka mitandaoni kama wanavyotaka lakini siyo sasa,” alisema Aunt Ezekiel. 

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.