Tuesday, November 10, 2015

MWANAMKAKATI WA LOWASSA ATIWA NDANI



Mwanamkakati wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bashir Awale, amekamatwa na kuwekwa ndani katika Kituo cha Polisi cha Kati.
Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya timu ya kampeni ya mgombea wa Chadema, Edward Lowassa, zinasema kuwa Awale alikamatwa juzi jioni kwenye maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Taarifa zaidi zinasema kuwa Awale alisimamamishwa na askari, ambao walimchukua kwenye gari lao huku wakilitelekeza gari lake kwenye maeneo hayo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alisema atalizungumzia suala hilo

leo pamoja na mambo mengine.
“Nimewaagiza vijana wangu waniandalie taarifa juu ya suala hilo. Nitalizungumzia jambo hilo kesho (leo) pamoja na mambo na mengine,” alieleza Kamishna Kova, ambaye hakutaka kuingia kwa undani wakati alipohojiwa kuhusiana na suala hilo.
kukamatwa kwa Awale kunahusishwa na masuala ya Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni kutokana na ukaribu wake na Lowassa

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.