Thursday, March 31, 2016

ANGALIA JINSI CHANGANYIKENI RANGERS WALIVYO MGEGEDUA MBUZI WA PASAKA.

Donoa donoa haikuwa ya kitoto kitu shaba kikawekwa katikati ya wana wakaanza kukifakamia fasta lakini kwakuwa hakukuwa na sahani ikabidi kitu kiwekwe kwenye sinia halafu wakakaa ma player kadhaa mkekani chombo kikapigwa kweupeee!. 
Ebanah eeh, hii ngoma ilikuwa ni pande za Changanyikeni Chadema na siku chache kama unakumbuka nilikutonya kuwa wana walimchukua mnyama huyu kwenye bonanza la Pasaka baada ya kumtundika Mbuyuni Fc kwa mikwaju ya Penati na kisha kukabidhiwa mwana Mbuzi huyu aliyenona ambapo hapa ndiyo wanamtafuna sasa.
Ebana eeh wahuni walikaa kivyao na Maplayer kivyao wakimgonga mwana Mbuzi kwa raha zao, cheki picha hapo.










No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.