Usiombe mvua inyeshe halafu uwe mtembea kwa miguu, Wakati barabara fupi kutoka Ubungo stendi ya mkoa mpaka Regho imepigwa mkeka safi pamoja na kuwa haina umuhimu wowote kituo kikuu cha daladala cha Mawasiliano hakifai kwenda wakati wowote, iwe jua au mvua.
Wakati wa jua kituo hiki huwa na vumbi kali na wakati wa mvua ndiyo hakifikiki kabisa, leo asubuhi kimetandazwa kifusi pekee lakini baada ya kunyesha mvua tu imekuwa ni shida kwa watembea kwa miguu na hata kwa wenye bodaboda na Bajaji. Ikiwa Serikali inabajeti ya kutosha kutokana na fedha za walipa kodi ambao kwa awamu hii wamekuwa wakibanwa kweli kweli nadhani ni wakati muafaka kwa Serikali kurekebisha barabara hiyo ili walipa kodi waone thamani ya huduma wanazostahili.
No comments:
Post a Comment