Inspekta Shedu anapewa kazi ya kumpeleleza Rose ambaye ni tajiri msifika nchini Razam. Pamoja na mali mbali mbali anazomiliki mwanamke huyu lakini pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa moja la kilokole nchini humo na mbunge aliye lazimika kuingia kwenye siasa ili kuficha maovu yake.....Je, pakoje, huyu hapa mkali wa hadithi za kipelelezi Shedrack Kilasi anashuka na kisanga kizima.
NNE unusu
mwanaume nilikuwa ndiyo natambuka hatua kwenye vidato vya ngazi nikilifuata
lango la kuingilia ofisini kwangu, wakati nachomeka ufungua na kuuzungusha
tayari kwa kufungua mlango mwili ukasisimka kidogo hii hutokea kunapokuwa na
jambo la hatari ama kheri akili ikanituma kugeuka naam, bila kungoja ikawa
hivyo.
Kitendo cha
kujipindua na kutupia jicho upande wangu wa kuume kwa umbali nikamuona mkuu wa
kazi yaani bosi wangu akinitazama huku akiwa amesimama tisti,baada ya kukata
sekunde kadhaa tukitupiana jicho akaonyesha ishara ya kuniita, yap,
nikauzungusha ufunguo kwa mara nyingine mlango ukafunguka mwanaume nikazama
ndani.
Baada ya
kuingia ndani nikaweka mizigo yangu mezani fasta halafu nikachomoka, hii
ilikuwa ni ndani ya dakika kama tano hivi ilipo timu ya saba nilikuwa ofisini
kwa mkuu wangu wa kazi.
“Naam mkuu,
habari ya kazi.” Nikasabahi.
“Salama,
vipi naona leo umejitahidi kuwahi mzigoni, una kazi nyingi sana?”
“No,sina
kazi sana zipo za kawaida ila basi tu leo nimejisikia kuwepo hapa mapema mkuu.”
Nikamwambia huku nikiifikicha mikono yangu kama niliyekuwa nikihisi baridi na
kweli ilikuwa hivyo kutokana na AC yam le ndani ilivyokuwa ikitema.
“Sasa,tulikaa
kama wakuu wa idara ya upelelezi tukulipitisha jina lako kufanya upelelezi wa
biashara za ile kampuni ya mchungaji Rose kama haihusiani na uuzaji wa dawa za
kulevya, lakini kingine kikubwa ni kuhusu huu uchungaji wake maana inasemekana
anatumia dini kutengeneza maisha yake na hivi karibuni ameingia kwenye siasa
ili kulinda biashara zake.” Kwa mara hii tena nikahisi mwili wangu ukisisimka.
Unadhani hadithi hii itoke mara ngapi kwa wiki?
tuma maoni yako kwenye namba: 0712 592 790 au shadrackkilasi@gmail.com
No comments:
Post a Comment