Hapa si Manzese ni sehemu ya barabara ya kuingia kituo cha Mawasiliano ambapo ukiacha mitumba ambayo huuzwa nyakati za jioni asubuhi hii vyombo vya udongo na plastiki humwagwa kila sehemu bila kujali vumbi kali ambalo linatokana na magari yanayopita sehemu hiyo.
Hapo ni mita tatu pekee kutoka barabarani hivyo ni rahisi mno kutokea ajali au uharibifu wa vyombo vyenyewe naamini wafanyabiashara kama hawa walistahili kutengewa sehemu tulivu zaidi tofauti na wale wa Mitumba.
Hata hivyo huu ni upuuzi wangu tu, ni wajibu wa Serikali kuufanyia kazi au kuupuuza.
No comments:
Post a Comment