AndalusiA,
Hispania
NDEGE ya kukodi iliyowabeba mabingwa wa
Ligi ya Europa, Sevilla imewasili jana asubuhi mjini Andalusia, baada ya
kuwachapa Liverpool mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja
wa St. Jakob Park mjini Basel, Uswisi.
Kundi la mashabiki lilikuwa likisubiri
katika Uwanja wa ndege wa San Pablo na kikosi hicho kilionyesha taji hilo kwa
mashabiki wao ambao walijawa na furaha isiyokifani.
Kikosi hicho hakitafanya sherehe hadi
watakapocheza fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Vicente
Calderon, Jumapili hii.
No comments:
Post a Comment