PARIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI Olivier Giroud, anataka
kuzungumza na Arsene Wenger juu ya nafasi yake kwenye kikosi cha Arsenal,
kufuatia mipango ya kocha huyo kutaka kuongeza mshambuliaji mwingine.
Taarifa mbalimbali zinadai kwamba,
Wenger na viongozi wa timu hiyo wanataka kumwaga kiasi kikubwa cha fedha kwa
ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Hispania, Alvaro Morata.
Imedaiwa kwamba Gunners wanataka kumwaga
pauni milioni 50 kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ili kuzifunika Manchester
City, Chelsea na Paris St-Germain zinazowania saini yake.
Kutokana na Danny Welbeck kupata
majeruhi yatakayomweka nje kwa miezi tisa, Wenger anataka kuingia sokoni kwa
ajili ya kunasa mshambuliaji mwingine.
Hivi karibunu kocha huyo, alisema: “Naamini
Danny Welbeck atakuwa nje kwa muda mrefu, tutakuwa njiani kuangalia
mshambuliaji mwingine."
Taarifa kutoka Ufaransa zinasema kwamba,
Giroud ameingia hofu kuhusu nafasi yake katika mipango ya Wenger ya msimu ujao,
hivyo anataka kukutana na kocha huyo kutaka kujua juu ya hatima yake.
Ingawa mshambuliaji huyo ana mkataba
kwenye klabu hiyo ya Emirates hadi mwaka 2018, lakini anataka uhakika.
No comments:
Post a Comment