Tuesday, June 21, 2016

HII NI TAMAA YA PESA WOGA?

Unayaona hayo magari yaliyoegeshwa hapo?
Hapo na chuo kikuu sehemu ya mlimani, sehemu hiyo hairuhusiwi kuegesha magari au pikipiki ukikamatwa umeingiza gari hapo unapigwa faini au unakamatwa na kupelekwa kituo cha polisi, tunafanyiwa hivyo waswahili siku zote.
Jumamosi ya wiki iliyopita licha ya sehemu za kuegesha magari nyingi kuwa wazi lakini jamaa waliamua kuvunja sheria zao wenyewe na kuruhusu magari kuegesha sehemu isiyoruhusiwa, waswahili tukajiuliza au kwakuwa ni ngozi nyeupe, tena badala ya kukamatwa yakawa yanalindwa kabisa, bado najiuliza sisi kwao tuna nafasi kama hiyo? Hata hivyo si kazi yangu kuyafanyia kazi haya na nijukumu lao kulichukua hili au kulipuuza, mi napita tu.





No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.