Ni wasomi kweli kweli, Maprofesa Madokta na wengine, ambao wanajua uwanja wa Chuo kikuu cha mlimani ni kwa ajili ya michezo lakini yapo maeneo ya wazi sehemu hiyo ambayo wanaweza kufanyia shughuli za kijamii tofauti na michezo.
Ni hawa hawa wasomi wetu ambao hufunga uwanja huo kwa ajili ya kuotesha nyasi na kutenga bajeti kwa ajili ya kuufanyia ukarabati uwanja huu.
Lakini unachotakiwa kuwashangaa na kutilia shaka uwezo wao wa kutafakari licha ya kuwa na maeneo ya wazi mengi sehemu hiyo ikiwemo ambayo hupewa Mchungaji
Mwakasege kwa ajili ya kufanyia maombi lakini wasomi wetu hawa jumamamosi na jumapili ya wiki iliyopita waliamua kwa moyo mkunjufu kuutumia uwanja wa mpira wa miguu kufanya shughuli za wachina lakini mbaya zaidi mwaka jana waliamua kuukodisha kwa waandaaji wa tamasha la nyama choma na shangwezikafanyika kwenye uwanja ambapo licha ya kuharibu nyasi uwanja ulikuwa na chupa kila sehemu.
Hata hivyo mimi nimeona hivyo ni jukumu lao kupuuza au kulifanyia kazi hapa.
No comments:
Post a Comment