Monday, August 1, 2016

ANGALIA PICHA ZA FAINALI YA TUJINOME CUP KIGAMBONI ILIVYOKUWA.

Ukiachilia mbali kuwepo na wanandinga wenye majina makubwa kama Said Morad lakini katika ndiki ya fainali iliyopigaka jana kwenye uwanja wa Mzimu uliopo katika kata ya Vijibweni pande za Kigamboni hatua kadhaa tangu mwisho wa lile daraja la Nyerere burudani zilifana sana.
Hata hivyo mtu wangu wa nguvu hapa nimekuwekea picha tu lakini kwa taarifa kamili usikose gazeti lako la Bingwa siku ya Alhamisi, kulinoga kweli kweli.

Lakini kilio cha Bw.George Malele mratibu wa mashindano haya ambayo ni kama Ndondo cup kasoro wenyewe wamekosa udhamini ni nini? Je, mwenyekiti wa taa wa Vijibweni bwana Jafary Athman anasemaje kuhusu mratibu wa mashindano haya kujitolea kuchangamsha kata hii hata pasipo kupata chochote na anamsaidia vipi, Diwani wa kata hii ambaye ndiye meya wa jiji anasemaje?
Tukutane alhamisi ndani ya Bingwa mtu wangu.












Mratibu wa michuano ya Tujinome Cup George Malele akipozi kwa ajili ya picha katika fainali ya michuano aliyoianzisha ambapo timu ya Burudani iliibuka bingwa na kujinyakulia mbuzi mnyama.

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.