LAGOS, Nigeria
AMA kweli mapenzi ni kikohozi hakiwezi kufichika.
Usemi huu unadhihirishwa na mwimbaji
nchini Nigeria, Augustine Miles Kelechi, maarufu jukwaani kama Tekno Miles, baada ya
kufunguka akielezea jinsi asivyoona wala kusikia dhidi ya mwigizaji, Genevieve Nnaji.
Staa huyo alifunguka mwishoni mwa
wiki, baada ya kutupia picha na ujumbe
kwenye mtandao wake wa Instagram akielezea hisia zake hizo.
Katika picha hizo,
ambazo zilimuonesha mwanamama huyo ziliambatana na ujumbe wa kusisitiza jinsi
alivyokufa na kuoza juu ya staa huyo.
“Penzi langu kwake daima halitakufa,” ulieleza
ujumbe ambao uliambatana na picha hizo.
No comments:
Post a Comment