Monday, November 21, 2016

STAA HUYU AOMBA AKATWE MGUU



LAGOS, Nigeria

MTUNZI na  mwandishi mahiri katika kijiji cha Nollywood, Segun Oke,  anaomba msaada kwa Wanigeria wa dola 20,000 ili aweze kusafiri kwenda  nchini India kwa ajili ya kukatwa mguu, baada ya mfupa wake kuathirika.

Hatua hiyo ni kutokana na kushindwa kupona, licha ya kufanyiwa upasuaji mara kadhaa tangu alipopata ajali ya gari mwaka 2003.

Akizungumza juzi, staa huyo, ambaye jina lake la uigizaji anafahamika kama Toyobo na ambaye alijijengea umaarufu kwa kipindi kilichotamba kwenye vituo vya televisheni, kiitwacho, Labe Orun, alisema kuwa kwa sasa hana jinsi, baada ya kushindikana kupona tangu alipopata ajali hiyo ambayo ilimwondoa kabisa katika tasnia hiyo.

“Baada ya siku tatu nikiwa hospitalini mguu wangu ulianza kuoza, baada ya hapo nikahamishiwa katika wodi maalumu ya mifupa ambako nilikaa kwa muda wa miezi sita kabla ya kuruhusiwa,” anaeleza staa huyo katika mahojiano na waandishi wa habari.


Alisema kuwa baada ya kuruhusiwa kutokana na kuwa yeye ndiye baba mwenye familia hakutaka kukaa kitandani na badala yake akaanza kutafuta msaada zaidi ambapo katika harakati hizo, mwaka 2013 alifanikiwa kukutana na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya mawasiliano ya Slot System, Nnamdi Ezeigbo, ambaye aligharimia safari ya kwenda India akafanyiwe upasuaji miguu yote miwili, lakini pamoja na kufanyiwa mguu wake mmoja hakuweza kurejea katika hali yake.
Alisema kuwa baada ya miaka miwili akiwa ameshaanza kuonekana kama atarejea kilingeni, lakini ukaanza kuuma tena ambapo kwa sasa hawezi hata kutoka nje.

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.