Thursday, August 29, 2013

HATIMAYE WENGER AMRUDISHA FLAMINI

Arsene Wenger amefanya usajili wa pili katika dirisha hili la usajili linaloelekea mwishoni kwa kumsajili kiungo wa zamani wa timu Mathieu Flamini kwa uhamisho wa bure kutoka AC Milan.
Kiungo huyo ambaye aliondoka Gunners mwaka 2008 kujiunga na  AC Milan,amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya  £40,000 kwa
wiki. Flamini, 29, ni mchezaji wa pili kusajiliwa baada ya mshambuliaji kinda wa kifaransa Yaya Sanogo, ambaye amejiunga na Arenal akitokea Auxerre bure. 
Flamini amekuwa akifanya mazoezi na Arsenal wakati wote wa pre season baada ya kuachwa na AC Milan mwishoni mwa msimu uliopita. 

No comments:

Post a Comment

KATUNI ZA MWAGITO HIZI HAPA MWANANGU.