Idadi ya watu waliofariki katika mashambulizi yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza, katika siku nne zilizopita, imefika watu miamoja.
Israel imefanya mashambulizi mengi sana nchini Israel tangu kuanza operesheni yake dhidi ya Gaza Jumanne kukabiliana na mashambulizi kutoka Gaza.Msemaji katika wizara ya afya eneo la Gaza, amesema kuwa katika mashambulizi ya
liyofanyika hivi punde, wanaume wawili wameuawa katika eneo la Bureij.
Mashambulizi yamefanywa kwa kutumia roketi, ambazo zililipua kituo cha mafuta Kusini mwa Israel katika mji wa Ashdod.
Roketi zimekuwa zikirushwa Kaskazini mwa Israel kutoka Lebanon kwa mara ya kwanza katika mzozo huu.
Jeshi la Lebanon limesema linajaribu kuchunguza kujua nani aliyefanya mashambulizi hayo.
Marekani imejitolea kusaidia pande hizo kwenye mgogoro kufikia mwafaka kutuliza vita.
Ripoti zinasema kuwa pamoja na wale waliouawa, watu 675 wengi wakiwa raia , wamejeruhiwa.
Hata hivyo Israel inasema kuwa ni wapiganaji pekee waliouawa.
No comments:
Post a Comment