LONDON, England
Nyota huyo wa Chile ambaye alionyesha kiwango kikubwa wakati wa fainali za Kombe la Dunia, ana uhakika kuwa klabu hiyo itabeba mataji mengine, baada ya kufunga msimu na Kombe la FA, Mei mwaka huu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona, anafikiri kuwa kuongezwa kwa Mesut Ozil katika kikosi hicho cha Arsenal, ndio kilichosaidia kunyakua taji msimu uliopita na msimu huu analipigia hesabu taji la Ligi Kuu England.
“Alipokuja (Mesut) Ozil katika kikosi hiki, Arsenal walikaribia kunyakua taji la Ligi Kuu England. Nina matumaini kuwa nitatoa mchango na kuweza kunyakua mataji mengine iwezekanavyo,” aliuambia mtandao wa klabu.
“Tuna kikosi kikubwa na ni klabu kubwa. Tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
“Kupata nafasi ya kucheza kila mara sio jambo kubwa lililonifanya nitue Emirates. Nimekuja hapa kunyakua mataji, Ligi ya Mabingwa Ulaya na ‘takataka’ zote.”
“Staili ya uchezaji wa kikosi hiki cha Arsene Wenger ni kama ile ya Chile. Hivyo naijua,” alisema. “Arsenal wanacheza vizuri sana na ndio staili ninayopenda. Hii ndio sababu kwanini nimekuja hapa.
“Niliambiwa ni kocha ambaye unaweza ukajifunza mambo mengi kutoka kwake. Anataka mafanikio makubwa kwenye soka, hilo ndilo limenisaidia kufanya maamuzi kusaini Arsenal.”
No comments:
Post a Comment