Na Mwandishi Wetu
BONDIA Ibrahimu Tamba ambaye ni bingwa wa uzito wa kg 72 ambaye ni bingwa wa TPBO anatarajia kuvaana na Baraka Mwakansope wa Mbeya mpambano wa ubingwa wa raundi kumi utakaofanyika january 30 katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM
akizungumzia mpambano huo promota Jafarri Ndame amesema siku hiyo kutakuwa na mipambano miwili ya ubingwa yote yakiwa na raundi kumi kila moja mpambano mwingine utawakutanisha Azizi Abdallah akatakaekabiliana na Selemani Zugo pia kutakuwa na mipambano mingine mikali ya utangulizi ambapo
bondiaTasha Mjuaji atapambana na Bakari Dunda na Jems Kibazange atacheza na Stivin Kobelo wakati Julius Kisarawe atapambana na Jems Martin na shomali Mirundi atakabiliana na Shedrack Ignas na Twaha Issa atakutana na Kassim Gamboo uku Husein Gobos akicheza na Samweli Stopa wakati Iddi Mgodomi atapambana na Shomari Punzi
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
No comments:
Post a Comment