Klabu ya Yanga imechukua uamuzi wa kuwashitaki wachezaji watatu moja kwa moja kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Yanga imetangaza kuwashitaki kipa Juma Kaseja, kiungo Mganda Emmanuel Okwi na mshambuliaji Jaja raia wa Brazil.Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Frank Chacha amesema leo wamechukua uamuzi huo kutokana na wachezaji hao kukiuka vifungu vya sheria.“Lakini pia tutaishitaki Simba kwa kuhusika kuvunja vifungu vya kisheria kutokana na kumshawishi Okwi kuvunja mkataba wetu,” alisema Chacha.
Jaja:
Yanga inasema alishindwa kurejea nchini kwa madai ana matatizo ya kifamilia. Lakini wanashangazwa kuwa hajarudi hadi leo na kuna taarifa amepata timu nyingine, hivyo wanashitaki.
Okwi:
Amekiuka sheria kwa kuvunja mkataba, wanaamini hakuwa sahihi na pia Simba ilimshawishi kuvunja mkataba nayo wanaishitaki.
Kaseja:Alishindwa kufuata vipengele vya kikatiba ikiwa ni pamoja na kutokwenda mazoezini wanadai bila ya kuwa na taarifa yoyote
No comments:
Post a Comment