ILIPOISHIA JUMATANO:
Vijana hao
wawili wakahuzunika sana na kutiririkwa na machozi ya hasira ikabidi wahadithie
mkasa ulio wakuta mpaka kwa nini wanahitajika kuuawa “katika familia yetu tuko
wawili tu mimi na mdogo wangu Davison(22)Baba na mama yetu walitupenda
sana,siku ya jumatano usiku wakati tumeketi sebureni na mama tukiwa na furaha
kupita kifani mara simu ya kiganjani ya mama ikawa inahita,mama akanyanyuka na
kusogeaa pembeni kidogo na kupokea simu
“hellooo….
”
SASA ENDELEA
NA FRANCISS MAIGE
“naongea na Mrs Ngowi…..????”mama
akaulizwa
“ndiyo mimi ujakosea”mama akamjibu
“mimi ni daktari mkuu kutoka hapa T.M.J nakuomba
ufike hapa mara moja mume wako amepata ajari mbaya sana”
“ samahani Daktari hiyo hospital yaT.M.J
iko sehemu gani……??”Mrs.Ngowi akamuuliza Daaktari
“T.M.J iko hapa mikocheni linatazamana
na jingo la May faiya plaza”Daktari akajibu
“sawa nimekuelewa nakuja hapo sasa hivi”
“okay akuna tatizo”daktari akakata simu
,
Mama akaingia chumbani kwake
akachukua pesa na mkoba wake huku akiwa amechanganikiwa akutaka kabisa sisi tufahamu kilicho
tokea,akatuaga na kuondoka kuelelea T.M.J hospital,kwa kuwa barabarani hapakuwa
na msongamano mkubwa sana wa magari Mrs.Ngowi akawahi kufika hospital akapita
mapokezi na kuuliza kuhusu mgojwa wake aliyeletwa leo anaitwa Mr.Ngowi ,dada wa
mapokezi akamuelekeza “ mume wako yuko katika chumba cha upasuaji inabidi
usubiri ,baada ya muda kidogo utapata ruhusa ya kumuona” Mrs.Ngowi akashusha
pumzi(mmmmh) na kuketi kwenye kiti kwa ajili ya kungojea taarifa kutoka katika
chumba cha upasuaji,baada ya muda mrefu kipita takribani dakika 55 kupita
Daktari akatoka katika chumba cha upasuaji na kumuita Mr.Ngowi ofisini kwake,Mr.Ngowi
akaingia ofisini kwa daktari huku akiwa na hofu kubwa moyoni mwake ikabidi
aketi hili apate taarifa kutoka kwa Daktari.Daktari akamsalimu Mrs.Ngowi na
kumueleza kila kitu kilicho mkuta Mr.Ngowi
“Mama pole sana kwa matatizo
yaliyotokea”
“asante tayari nimeshapoa..kitu gani kimemkuta
mume wangu”Mrs.Ngowi akamuuliza Daktari
“mumeo amepata ajari mbaya sana iliyo
sabishwa na gari aina ya roli na kugonga gari yake ameumia sana maeneo ya
kichwani, alipofikishwa hapa tukampokea na kumpeleka katika chumba cha upasuaji
kwa kuwa aliumia sana kichwani,tumefanikiwa kumsaidia na tumejitahidi sana
kuokoa maisha yake lakini…”
Mrs.Ngowi
akapatwa na mshangao kuona Daktari anasita kumueleza ukweli wa mambo,ni kitu kimetokea
katika chumba cha upasuaji ikabidi avue roho ya uwoga na kuvaa ujasiri hili
apate ukweli kutoka kwa Daktari.
No comments:
Post a Comment